- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAORODHESHA VITAMBULISHO 8 KUMTAMBUA MPIGA KURA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo ametangaza rasmi uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika ngazi ya mtaa, kijiji na kitongoji unatarajiwa kufanyika Novemba, 24 mwaka huu.
Jafo ametaja kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambazo zimeainisha aina 8 za vitambulisho ambavyo msimamizi wa kituo cha uchaguzi anaweza kumtaka mpiga kura aonyeshe ili kujiridhisha kama jina lake ndilo liko ktk orodha ya mpiga kura.
Kanuni hizo zimetaja kitambulisho cha mpiga kura, cha kazi, hati ya kusafiria, kadi ya bima ya afya, cha shule au chuo, cha mfuko wa hifadhi ya jamii, leseni ya udereva na kitambulisho cha Taifa kuwa vyote hivyo vinaweza kutumika.
Akitoa tangazo la uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2019 katika Ofisi za TAMISEMI zilizoko katika eneo Mtumba Jijini Dodoma Mhe. Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kuhakikisha wanazingatia miongozo na kanuni za uchaguzi huo.
Mhe. Jafo amesema kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 ibara 4(1-3), Matangazo ya Serikali Na. 371, 372, 373 na 374) ya mwaka 2019, Waziri mwenye dhamana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anautangazia umma wa Watanzania na Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu kuwa tarehe 24 Novemba, 2019 itakuwa ni siku ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara.
“Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kifungu cha (1) Waziri mwenye thamana na serikali za mitaa anapaswa kutoa Tangazo la Uchaguzi kwa Umma si chini ya siku 90 kabla ya siku ya uchaguzi”. Anafafanua Mhe. Jafo
Mhe. Jafo anaeleza zaidi kuwa tarehe hiyo imepangwa baada ya kukamilika kwa kanuni ambazo zitatumika kuendesha uchaguzi huo ambapo wadau, vyama vya siasa na asasi za kiraia zilishirikishwa na kutoa maoni yao.
“Uchaguzi wa mwaka huu, utakuwa bora, kwasababu umekuwa shirikishi wakati wa uandaaji kanuni na tumeandaa kanuni ambazo zinaondoa changamoto zilizokuwa zikijitokeza kwenye chaguzi zilizopita” Amesema Mhe. Jafo