Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 2:17 pm

NEWS: SEREKALI YAONGEZA SIKU 3 ZA KUJIANDIKISHA UCHAGUZI SEREKALI ZA MITAA

Dar es salaam: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ametangaza fursa ya kuongeza siku tatu za uandikishaji wa wapiga kura katika orodha ya daftari la mpiga kura kwaajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 24 Novemba, 2019.

Wazari Jafo ametoa kauli hiyo leo jumapili Octoba 13, 2019 mara baada ya kujiandikisha kwenye Orodha ya Daftari la Mpiga kura kwenye Kitongoji cha Kimani Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.

Oktoba 11, akiwa mkoani Katavi kwenye ziara ya kikazi ya Rais wa Tanzania, John Magufuli, Waziri Jafo aliahidi kupeleka mapendekezo maalumu kwa Rais kuomba mikoa itakayofanya vibaya iongezewe muda wa uandikishaji.

Jana Oktoba 12, Rais Magufuli alisema mikoa ambayo viongozi wake watashindwa kuwahamasisha wananchi kujiandikisha ili wapige kura atawashangaa huku akisema hadhani kama atalaumiwa na Watanzania kwa hatua atakazozichukua,kauli hiyo aliitoa jana wakati wa uzinduzi wa safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) mkoani Katavi, “Waziri (Jafo) ametoa takwimu za baadhi ya mikoa iliyofanya vizuri. Ninafuatilia lakini alitoa iliyofanya vibaya, mchakato ukikamilika nitataka anipe taarifa ya mikoa iliyofanya vizuri na vibaya,” alisema Rais Magufuli kwenye ziara hiyo.