- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAMUAGIZA IGP SIRRO KUPELEKA WACHUNGUZI NJOMBE
Iringa: Naibu waziri wa mambo ya Ndani ya nchi HAMAD MASAUNI amemtaka Inspecta genarali wa Jeshi la polisi nchini (IGP) SIMON SIRRO kutuma timu ya wataalamu mbali mbali mkoani Njombe ili kusaidiana na jeshi la polisi mkoani humo kupambana na vitendo vya utekaji na ukatili wa mauji ya watoto wadogo.
Agizo hilo limetolewa mkoani Njombe wakati waziri wa mambo ya Ndani akizungumza na waandishi wa habari na kutoa tathmini ya ziara yake ya siku tatu mkoani mkoani humo yenye lengo la kupambana na mauaji dhidi ya watoto wadogo yanayoendelea mkoani Njombe.
“Namuelekeza IGP kwanza kutuma timu ya wataalamu wa aina mbalimbali kutoka makao makuu ya dar es salaamu waje Njombe mara moja kwa dhamira ya kwanza kuongeza Nguvu kwa jeshi la polisi mkoa wa Njombe kukabiliana na haya majanga lakini kuweza kushirikiana nao kwa kuweza kuwahoji wale ambao tayali wameshikiliwa na polisi kutokana na tuhuma hizi ili tuweze kupata uthibitisho wa mtandao mzima kupitia kwao kusudi wote waliohusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wahalifu wengine popote pale nchini” alisema naibu waziri wa mambo ya Ndani
“ Na pili kuongeza nguvu ya dolia na operation ya misako hususani katika maeneo ya misitu kwa kushirikiana na wadau mbali mbali”
waziri amesema kuwa jeshi la polisi lilitumia mabomu ya machozi ili kumsaidia kijana aliyekuwa akiadhibiwa na wananchi kwa kosa la kuingia katika moja ya nyumba mjini hapo kwa dhamira ambayo bado haijajulikana.
“katika uchunguzi wangu nilibaini kuwa kijana Yule aliingia katika nyumba ya mama mmoja kwa dhamira isiyojulikana wakati mama mwenye nyumba hayupo na majirani walipomwona wakamfungia kwa nje ndipo yeye akachukua uamuzi wa kupanda ukuta na kujaribu kutaka kutoroka ndipo wananchi walipomfukuza na kutaka kumpiga huku wengine wakidhani huyo pia ni miongoni mwa watu wanaohusika na utekaji wa watoto na kwamba alikwenda kule kwa dhamira ya kuteka mtoto, na wananchi wakaanza kuchukua sheria mkononi jeshi la polisi likachukua hatua sasa za kumchukua Yule mtuhumiwa ili kumpeleka kituoni ndipo taharuki ilipotokea”aliongeza Waziri Masauni