Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:32 pm

NEWS: SEREKALI YAMPINGA RC HAPI KUHUSU VITAMBULISHO VYA MACHINGA

Serekali kupitia Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa (TAMISEMI) Mwita Waitara amesema maagizo anayoendelea kuyatoa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi kuhusu makundi yanayotakiwa kupewa vitambulisho vya WAMACHINGA si ya Serikali.

“Tamko linaloendelea kuzunguka katika mitandao ya jamii na vyombo vya habari likimhusisha mkuu wa mkoa wa Iringa sio maelekezo ya Serikali.

“Hivyo ninatoa wito kwa wakuu wote wa mikoa, watendaji wote kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na serikali kuhusu ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara na watoa huduma wadogo,” amesema.

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa Mei 31 2019 bungeni Jijini Dodoma na Waitara baada ya wabunge kupitisha bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 2019/2020.

Waitara amesema katika kikao cha Rais John Magufuli, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wakuu wa mikoa wa Tanzania Bara, alitoa vitambulisho 650,000 kwa wakuu wote wa mikoa kwa awamu ya kwanza. Amesema kwa awamu ya pili, alitoa vitambulisho milioni 1.2 na hivyo kufanya jumla ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa kufikia milioni 1.85.

Waitara amesema ili kupata vitambulisho hivyo, wafanyabiashara na watoa huduma wadogo wanatakiwa kulipa Sh20,000 kwa kitambulisho kimoja. Amesema lengo la Serikali ni kuwatambua wafanyabiashara wadogo na watoa huduma wadogo ambao mauzo ghafi yao hayazidi Sh4milioni kwa mwaka.

Amezitaja sifa za mfanyabiashara anayetakiwa kupewa kitambulisho awe na mapato ghafi yasiyozidi Sh4milioni kwa mwaka, awe hajawahi kuandikishwa na kupewa namba ya kitambulisho cha mlipa kodi (TIN).

Amesema hadi kufikia Mei 26, jumla ya vitambulisho milioni 1.85 vimegawiwa kwa wakuu wote wa mikoa Tanzania Bara. Waitara amesema vitambulisho 1,176,305 vimegawiwa kwa wafanyabiashara na watoa huduma wadogo na tayari Sh23.5 bilioni zimekusanywa. Amesema ili kuboresha kazi hiyo, Serikali imekamilisha mwongozo wa ugawaji wa vitambulisho hivyo na utaanza kutumika mwaka wa fedha 2019/2020.

Hili ndilo agizo na maelekezo ya RC Hapi kuhusu wanahabari lakini baadae aliufuta