- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YALIFUNGUA KANISA LINALOMSUJUDIA MCHUNGAJI WA KIKE
Mwanza. Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk Philis Nyimbi amesitisha ibada katika kanisa la mchungaji Bi. Diana Bundala maarufu Mfalme Zumaridi lililopo mtaa wa Iseni kata ya Butimba wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.
Uamuzi wa kulifunga kanisa hilo umetolewa jana Jumatatu Novemba 18, 2019 baada ya kuwepo kwa malalamiko ya watu mbalimbali kuhusu ibada za mhubiri huyo ambaye pia hujiita Mungu wa duniani.
Baada ya amri hiyo kutolewa mchungaji huyo hakuwa tayari kueleza chochote.
"Mimi sina cha kusema. Siwezi kuzungumza chochote kwa sasa," amesema mchungaji Diana alipotakiwa kutoa maoni yake
“Serikali imebaini kiongozi wa kanisa hili anaendesha ibada kinyume na sheria ya usajili wa vyama au jumuiya za kijamii sura 337 kwa kupotosha umma kwa kujiita Mungu wakati yeye ni binadamu au baba na mfalme wakati yeye ni mwanamke.”
“Kwa mamlaka niliyopewa kwenye sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997 kifungu cha 14, 15, 16, vinavyosema punde tunapobaini kikundi au taasisi ina viashiria vya uvunjifu wa amani, mara moja tunapaswa kuchukua hatua, nasitisha shughuli zote za ibada kanisani na nyumbani kwa mchungaji Diana,” amesema Dk Nyimbi.
“Kiongozi wa Kanisa hili anajiita baba na mfalme wakati yeye ni wa jinsi ya kike,” amesema Dk Nyimbi.
Amesema baadhi ya vitendo ambavyo hata hivyo hakuvitaja vinavyofanywa na kiongozi wa kanisa hilo vina athari na madhara kwa waumini na watu wengine