Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:34 am

NEWS: SEREKALI YAKIRI KUZUILIWA KWA BOMBADIER NCHINI CANADA

Dar es salaam: Serekali kupitia kaimu Msemaji mkuu wa Serekali Bi Zamaradi Kawawa Imekiri kuzuiliwa kwa ndege yake aina ya Bombadier nchini kanada iliyokuwa ikiagizwa na serekali ya Tanzania, katika taarifa yake Bi Kawawa amesema kuwa ndege hiyo imezuiliwa kufuatiwa kuwepo na mgogoro uliotengenezwa na Wanasiasa wa Kitanzania ili kumkomesha Rais Magufuli,

"Mgogoro huo upo ila kimsingi mgogoro huo umetengenezwa na watanzania wenzetu, ambao kwa bahati mbaya sana wameweka maslahi ya kisiasa na ya kibinafsi mbele badala ya kuweka mbele maslahi ya taifa." aliongea Bi Kawawa


kauli hiyo imekuja baada ya Mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu kuzungumza na waandishi wa habari na kudai kuwa ndege ya Bombadier ilikuwa inatarajiwa kufika nchini mwezi uliopita imekamatwa na kampuni ambazo zinaidai Serikali ya Tanzania


Bi Kawawa amekiri kuwepo kwa zuo hilo ambalo linataka ndenge hiyo isiondolewa mpaka hapo kesi ya msingi itakapo malizika, sasa kulingana na zuio hilo serekali imedhamiria kuchukua hatua kadhaa ambazo moja ni hatua za kidiplomasia na hatua za kisheria ili kumaliza jambo hilo, PIli serekali imedhamiria kuwachukulia hatua kwa wale wanao shabikia na kutengeneza migogoro na hujuma mbalimbali dhidi ya nchi ya Tanzania nakusema kuwa serekali inawafatilia myenendo yao.

Aidha Bi Kawawa amesema kuwa Serekali ilikuwa na taarifa ya kuwepo kwa wanasheria waliofungua kesi dhidi ya Tanzani wakiomba Ndege hiyo(Bombadier) Ishikiliwe

"kunaviongozi wa baadhi ya vyama vya siasa ambao kwa namna moja au nyingine wangependa kuhujumu jitihada za Rais Magufuli zakuwaletea watanzani maendeleo, Wanasheria hao ambao walishinikizwa kwa taarifa tulizonazo, na baadhi ya wanasiasa wetu, walikwenda kufungua madai yakwamba serekali inadaiwa na kuomba ndege hiyo ishikiliwe, hawana uhalali wowote wakufanya hivyo na wamesukumwa na baada ya wanasiasa" alisema Bi Kawawa.

Imeandikwa na Deyssa h, Issa