Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:44 am

NEWS: SEREKALI YAKATA RUFAA UWAMUZI KUMUACHILIA HURU TIDO MHANDO

Dar es salaam: Serekali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imekata rufaa kupinga uwamuzi uliotolewa na Mahakama ya hakimu mkazi kisuti ya Kumuachilia huru aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando.

Mahakama hayo ilifanya maamuzi ya kumuachilia Mhando chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi ambaye alisema sababu za kumwachia huru kuwa ni mikataba minne aliyoingia haikuwa na nguvu ya kisheria kwani haikusainiwa na wahusika akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Lakini Jamhuri wanadai mashtaka yao ni hayo hayo kwamba mikataba hiyo iliingiwa bila kufuata utaratibu.

Pia wanadai kwamba kuingiwa kwa mikataba hiyo isiyofuata utaratibu kulisababisha Kampuni ya Channel Two Group kufungua kesi na Serikali ikalipa mawakili Sh milioni 887.1 ambayo ni hasara iliyosababishwa na mshtakiwa.

Katika kesi hiyo Tido alikuwa anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 887.1.