Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:29 am

NEWS: SEREKALI YAKATA RUFAA HUKUMU YA MALINZI

Dar es salaam: Serikali ya Tanzania imewasilisha nia ya kukata rufaa Mahakama Kuu, kupinga hukumu na adhabu iliyotolewa na Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, dhidi ya aliyekuwa rais wa zamani wa TFF, Jamal Malinzi na katibu wake, Celestine Mwesigwa.

Malinzi na Katibu huyo Desemba 11 mwaka huu walihukumiwa kifungo cha miaka miwili kwenda Jela au badala yake kulipa faini ya Tsh 500,000 na Mwesigwa Shilingi miliomi 1.

Mahakama hiyo ilitoa hukumu hiyo baada ya kuwatia hatiani wawili hao. Wakati Malinzi akitiwa hatiani kwa shtaka moja la kutengeneza nyaraka za uongo, Mwesigwa alitiwa hatiani kwa kutumia nyaraka hizo.

Hata hivyo Mahakama hiyo iliwaachia huru washtakiwa wawili katika kesi hiyo ambao ni aliyekuwa mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Frola Rauya ambaye alikuwa karani.

Katika shtaka hilo Malinzi anadaiwa kutengeneza nyaraka hizo zinazoeleza kuhusu kikao cha kamati tendaji ya TFF kwa kubadili watia saini badala ya Edagar Masoud aliwekwa Mwanga. Katika kesi hiyo ya jinai namba 213/2017 washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 20 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha ambazo ni Dola 173,335 za Marekani.