- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAIPINGA KESI YA JOSHUA NASSARI MAHAMAKANI
Dodoma: Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imepanga kutolea uamuzi wa mapingamizi matatu ambayo yamewekwa na upande wa Serikali katika kesi ya maombi madogo ya kufungua kesi msingi kwa ajili ya kutengua uamuzi wa Spika wa Bunge wa kumfutia ubunge aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari.
Nassari alifungua Maombi madogo ya kupinga hatua ya spika wa bunge Kumfuta kwenye nafasi ya Ubunge Machi 20 mwaka huu.
Jaji Latifa Mansoor anayesikiliza kesi hiyo namba 22 ya mwaka 2019 ameahirisha kesi hiyo leo hadi Machi 29 mwaka huu kwa ajili ya kusikiliza mapingamizi hayo ambayo hata hivyo hayakutajwa mahakamani hapo.
Maamuzi hayo yanakuja baada Mahakama kupokea mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa Serikali ukiwakilishwa na mawakili wawili ambao ni Alisia Mbuya na Masunga Kawahanda.
Jaji aliagiza pia kusifanyike uchaguzi wowote jimboni hadi hapo maombi hayo yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi. Nassari ambaye alikuwepo mahakamani hapo amewakilishwa na mawakili wawili Hekima Mwasipe na Fred Kalonga. Hata hivyo Jaji ameieleza mahakama kuwa shauri hilo litasikilizwa tena Machi 29, 2019 kwa ajili ya uamuzi wa mapingamizi hayo ya upande wa Serikali