- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAIPA MWEZI 1 KAMPUNI YA BSS KUMLIPA MSHINDI 2019 MILIONI 50 ZAKE
Serekali ya Tanzania imetoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Kampuni ya Benchmark Production inayoendesha mashindano ya kusaka vipaji kwa wasanii wa muziki nchini Tanzania Bonga Star Search (BSS) kuhakikisha wamemlipa mshindi wa kwanza wa mwaka 2019 zawadi yake ya milion 50 kama ilivyotangazwa.
Agizo hilo limetolewa leo Aprili 8, 2020 na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma ambapo ameitaka kampuni ya Benchmark 360 Ltd ambao ni waandaji wa mashindano ya kutafuta vipaji ya BSS KUMLIPA milioni 50 Mshindi Ndg. Meshack Fukuta ndani ya mwezi mmoja kuanzia hii leo.
Meshack aliibuka mshindi kwenye mashindano hayo yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo kampuni ya Benchmark walitakiwa kumlipa mshindi kiasi cha shilingi milioni 50 ambapo kati ya hizo, milioni 30 ni kwa ajili ya usimamizi na promotion na milioni 20 alipaswa kukabidhiwa mkononi. Hata hivyo hadi kufikia leo Benchmark hawajamlipa Ndg. Meshack jambo lililopelekea kuleta malalamiko yake kwa Naibu Waziri.
Naibu Waziri amesisitiza kuwa endapo kampuni ya Benchmark ambayo inaongozwa na Mkurugenzi wake Madam Rita Pousen haitokamilisha malipo hayo ndani ya mwezi mmoja basi hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuyafungia mashindano