- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAHAIRISHA UJENZI WA BARABARA YA DAR - CHALINZE
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, amesema Serekali imeahirisha ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam hadi Chalinze yenye urefu wa kilometa 144 kwa kiwango cha 'expressway' hadi miradi mingine inayoendelea itakapokuwa imekamilika.
Akiwasilisha bungeni jana hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, alisema mradi huo pia unahusisha ukarabati kwa kiwango cha lami sehemu ya Mlandizi - Chalinze unaofanyika kwa awamu na hadi Machi mwaka huu, mkataba kwa ajili ya ukarabati wa kilometa 12.4 ulikuwa umetiwa saini na maandalizi yanaendelea.
Alisema barabara ya Kwa Mathias-Msangani (Km 8.3) kwa kiwango cha lami upo katika hatua ya ununuzi
Waziri Kamwelwe alisema upambuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Morogoro – Dodoma yenye urefu wa Km 260 taratibu kwa ajili ya kumpata mhandisi mshauri wa kufanya kazi hiyo zinaendelea.
“Ujenzi wa Barabara ya New Bagamoyo (Morocco) Junction Mwenge - Tegeta yenye urefu wa Km 17.2 hadi Machi, mwaka huu, mkataba wa upanuzi wa sehemu ya Morocco na Mwenge Km 4.3 ulikuwa umetiwa saini kwa ufadhili wa Serikali ya Japan," alisema. Katika hotuba yake hiyo, Waziri Kamwelwe pia aligusia ujenzi wa barabara za juu (flyover/interchange na maboresho unaoendelea katika Jiji la Dar es Salaam.
Alisema ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya Tazara umekamilika huku ile ya makutano ya Ubungo ukiwa umefikia asilimia 28. “Kazi ya uhamishaji wa miundombinu iliyoathiriwa na mradi wa Ubungo Interchange imekamilika na mkandarasi anaendelea na ujenzi wa barabara za makutano," alisema.