Home | Terms & Conditions | Help

November 21, 2024, 9:44 pm

NEWS: SEREKALI YAFUNGULIA MAGAZETI MANNE

Dar es salaam. Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari hapa nchini Nape Nnauye ameyarudishia leseni magazeti manne ambayo yalikuwa yamefungiwa kwenye utawala wa Rais John Pombe Magufuli.

Waziri Nape ametoa leseni hizo hii leo Februari 10, 2022 wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali ya habari .

Magazeti yaliokuwa yamefungiwa ni Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima linalomilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

"Agizo la Rais ni sheria na inapaswa kutekelezwa, leo nitatoa leseni kwa magazeti manne yaliyokuwa yamefungiwa ambayo ni Mwanahalisi, Mawio, Mseto na Tanzania Daima kwa sababu ni vizuri kuondoka kwenye maneno tufanye vitendo hivyo tuanze na ukurasa upya sasa mwenye maneno yake aseme mwenyewe, kifungo kimetosha kikubwa kazi iendelee”. Amesema waziri huyo.

Pia, Waziri Nape ameagize Idara ya Habari Maelezo kwa kushirikiana na wahariri na taasisi zingine za habari ndani ya muda mfupi kuandaa kikao cha wadau wa habari kujadili marekebisho yaliyopelekwa Serikalini ya sheria ya habari.

“Kwenye hicho kikao mwisho wake tutatengeneza kamati ndogo ambayo itatokana na waandishi wa habari tushauriane tupitie kifungu hadi kifungu tuone ni namna gani wapi tunakubaliana halafu tupeleke marekebisho bungeni ya kupitia upya sheria ya habari' amesema waziri Nape