- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAFANYIA MABADILIKO SHERIA YA TAKWIMU HARAKA HARAKA
Serekali imefanyia mabadiliko Sheria ya Takwimu, marekebisho yaliyolenga kwenye vifungu vya haki ya kuchapisha au kutoa taarifa za takwimu kwa umma
Mabadiliko hayo yalifanywa na Bunge jana kupitia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, Namba 3 wa Mwaka 2019, uliowasilishwa kwa hati ya dharura.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Prof. Adelardus Kilangi, alisema mapendekezo hayo yanakusudia kuanzisha Kamati ya Kitaalam (Technical Committee) ambayo jukumu lake litakuwa kupokea kujadili malalamiko yanayotokana na wadau kuhusu usahihi wa takwimu zilizotolewa kwa umma.
“Katika jedwali la marekebisho, inapendekezwa kufuta vifungu vya 24A na 24B na kuviandika upya, pia kuongeza vifungu vipya vya 24C, 24D, 24E na 24F kwa lengo la kuweka utaratibu wa kutoa matokeo ya takwimu zinazotofautiana na takwimu rasmi zilizotolewa na serikali,”alisema Kilangi.
Alisema marekebisho hayo yanatoa fursa kwa mtu yeyote kutoa takwimu zinazotofautiana na zilizotolewa na Serikali, iwapo atakuwa amezingatia misingi ya kitakwimu iliyowekwa katika miongozo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa inayosimamia utoaji wa takwimu.
Sambamba na marekebisho hayo sheria hiyo inapendekeza kufutwa kwa kifungu cha 37 (4) kinachotoa adhabu kwa mtu anayetoa taarifa za takwimu bila kupata kibali cha Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).