- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAFAFANUA WANAOTAKIWA KUVAA MASK KUZUIA CORONA
Serekali imesema kuwa katika Kipindi hiki cha kuenea kwa ugonjwa wa Corona si kila mtu anapaswa kuvaa mask(Barakoa) au kuvaa kiholela, Mask zinawatu wake wanao paswa kuvaa na Muda wake pia wa kuivaa.
Akifafanua juu ya hali hiyo jana Machi 18, 2020 Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Udhibiti na Ufuatiliaji wa Magonjwa Mlipuko, Dk. Janeth Mghaba amesema kifaa hicho kinavaliwa si zaidi ya saa nne tu na mtu ambaye tayari ana maambukizi kusudi asimuambukize mwingine.
Amesema hiyo ni kwa sababu siyo rahisi mtu akakohoa aidha kwa kutumia kiwiko au mkono atakuwa na maji maji na mara nyingi ataweza kumuambukiza mwenzie.
“Kwa hiyo yule ambaye ni mgonjwa tu, tunasema kwamba ukijisikia dalili za kukohoa basi wewe vaa mask yako nenda kwenye kituo cha afya karibu au hospitali.
“Mask pia zinaweza kuvaliwa kwenye sehemu za msongamano au sehemu zenye watu wengi lakini kwa sababu tayari serikali imeshapiga marufuku hii misongamano, hatutegemei kukuona wewe unavaa mask unapita sehemu ambako hakuna msongamano na wewe ni mzima huna maambukizi,” amesema.
Aidha, Dk. Mghaba amebainisha kuwa kuna hatari kubwa ya kuvaa mask kwa sababu watu wengi bado hawajawahi kuuzingatia uvaaji wake.
“Mask hizi zinatakiwa kuvaliwa kila baada ya saa nne na kuzibadilisha, usipokuwa na hii tabia ya kuzibadilisha ukakaa nayo siku nzima kwako wewe ni hatari, itakuletea maambukizi mengine zaidi. Kwa hiyo tunashauri matumizi haya ya uvaaji mask yawe yanatumika kwa usahihi,” amesema.