- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAANZA UCHUNGUZI KUTOWEKA KWA MDUDE CHADEMA
Pia Masauni ameomba wananchi wote kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola kuhusu utata wa tukio hilo.
Kauli hiyo ya Masauni imeitoa leo Bungeni May 6, 2019 baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, kuitaka Serikali kufuatilia na kutoa taarifa za kutekwa kwa Mdude Nyagawa ambaye anadaiwa kutekwa
Mdude anadaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana kwenye ofisi yake Mbozi, mkoani Songwe juzi, Mei 4, 2019 wakiwa na silaha za moto.
Chenge ametoa maelekezo wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliyetoa hoja ya kuahirisha Bunge kwa kutumia kanuni ya 64 kuhusu kujadili jambo la dharura.
Katika hoja yake, Msigwa alisema hivi karibuni kumekuwapo na matukio ya watu kutekwa, kupotea na hata kuuawa, huku akitolea mfano madai ya kutekwa kwa kada wa chama hicho, Mdude.
“Ni kweli suala lolote linalohusu uhai wa binadamu, itakuwa vizuri Serikali itoe maelezo ili wananchi wajue hali ilivyo,” amesema Chenge.