- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAANGUKA KWENYE KESI YA SHERIA YA HABARI NCHINI
Arusha: Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) imetoa hukumu juu ya Kesi iliyofunguliwa na Baraza la habari Tanzania(MCT), Kituoa cha sheria na haki za binaadamu nchini juu ya baadhi ya vipengele vilivyopo katika Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 inakiuka uhuru wa kujieleza na vinapingana na Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na sheria za kimataifa ambavyo Tanzania imeridhia kwahiyo mahakama hiyo imeitaka serekali ya Tanzania kuvibadilishaa vipengele hivyo.
Katika hukumu iliyosoma leo Alhamisi Machi 28, 2019 kwa muda wa takribani saa 2:06 na Jaji Charles Nyachae wa kitengo cha awali cha EACJ akiwa na Jaji Kiongozi, Monica Mugenyi na Jaji Audice Ngiye, ameitaka Serikali kuvifanyia mabadiliko vipengele vya sheria hiyo ili kulinda uhuru wa kujieleza na haki ya kupata habari nchini Tanzania.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Baraza hilo la Habari Tanzania (MCT), Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) waliokua wakitetewa na mawakili, Fulgence Massawe, Jebra Kambole, Mpale Mpoki , Donald Deya na Jenerali Ulimwengu.
Mahakama ya EACJ imekubaliana na walalamikaji kuwa vifungu katika sheria ya Huduma ya Habari vya (3)(a), 13, 1920, 21, 34 pamoja na vifungu vingine vinakiuka utawala bora, demokrasia na utawala unaozingatia sheria na inapingana na mkataba ulioanzisha EAC. Mara baada ya hukumu hiyo, Wakili kiongozi wa waleta maombi, Fulgence Massawe amesema ushindi huo ni wa kihistoria na unathibitisha hoja za wadau mbalimbali walizokua wakisema sheria hiyo siyo nzuri kwa maslahi mapana ya nchi.