- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YAAHIDI KUENDELEZA KUYAFANYA MAZURI YOOTE YA DKT MENGI
Kilimanjaro: WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali itaendelea kuyaenzi aliyokuwa akiyafanya aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dk.Regnald Mengi aliyezikwa nyumbani kwake Kisereni, Kijiji cha Nkuu Sinde, Wilaya ya Hai.
Maelezo hayo Waziri mkuu aliyatoa jana wakati akiwaongoza maelfu ya watu katika shughuli ya kuhitimisha safari ya mwisho duniani ya Dkt Mengi.
“Huu ni msiba mkubwa, mzito kwa kumpoteza kama ambavyo baba Askofu Mkuu (Dk. Shoo) kasema. Huyu mzee Mengi ni mmoja wa watu wazalendo kabisa kutokea katika historia ya nchi yetu. Nimuombe Mwenyenzi Mungu aendelee kutupa nguvu ya kumsindikiza katika nyumba yake ya milele,” alisema Waziri Mkuu
Akitoa salaam za serikali katika ibada ya mazishi ya Dk. Mengi, Majaliwa aliwaeleza waombolezaji kuwa amekuja Kilimanjaro na salaam kutoka kwa Rais Dk. John Magufuli na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ambao wote wanawaombea, lakini wanawapa pole kwa msiba huo mzito.