Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 7:44 am

NEWS: SEREKALI YA UINGEREZA YAZUIA DHAHABU YA DOLA $1.2B YA VENEZUELA

Benki kuu ya nchini Uingereza imewazuia maafisa wa serekali ya Venezuela ambao ni wasaidizi wa Rais Nicolas Maduro kutoa dhahabu yenye thamanai ya dola bilioni $1.2 waliyokuwa wameihifadhi kama pesa ya akiba ya njee(foreign reserves ) kwa nchini hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa nchini Uingereza inasema kuwa nchini hiyo imechukua uamuzi huo ili kumdhibiti Maduro anayehangaika kuendeleza utawala wake nchini Venezuela

Nchi ya Uingereza imeungana na Marekani kumtambua mpinzani mkuu wa kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Urais Bw. Guido kama rais wa mpito wa Venezuela

Kulingana na taarifa iliyochapishwa na CNN inasema kuwa kiasi hicho cha gold ni miongoni wa pesa ya akiba ya njee(foreign reserves ) ya dola Bilioni $8 inayomiliki nchini hiyo.

Mwishoni wa wiki hiii umoja wa ulaya ulimtaka Bw. Maduru kuitisha uchaguzi wa Marudio ndani ya siku 8.

Juzi serekali ya Venezuela ilifunga mahusiano baina yake na Marekani baada ya Rais Trump kumtambua mpinzani wake kama ndiye Rais wa Nchi hiyo

Nchi ya Venezuela kwa sasa imejawa na maandamano ya kumpinga bw. Maduru kufuatia Ushindi aliyoupata mpinzani wake