- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI YA TANZANIA YAMWITA MWAKILISHI WA WHO KUHUSU EBOLA
Serikali ya Tanzania imefanya mazungumzo na mwakilishi mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu uchunguzi wa ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Kwa mujibu wa ukurasa wa Twitter wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dkt Hassan Abbasi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro ndiye aliyekutana na mwakilishi mkaazi wa WHO nchini Tanzania Dkt Tigest Katsela Mangestu.
Kwa mujibu wa Dkt Abbasi serikali imemwita Dkt Mangestu ili kupata undani wa hoja za shirika hilo ambazo zimeripotiwa na vyombo vya habari.
Dkt Abbasi pia amedai kuwa katika mazungumzo hayo, "WHO imeafiki kuwa kama kuna mahitaji ya kupata taarifa zaidi kutoka Serikali ya Tanzania lazima utaratibu ulioanishwa katika miongozo ya taasisi hiyo na ambayo imeridhiwa na Serikali ifuatwe kikamilifu."
Katika taarifa yake ya malalamiko, shirika hilo limeeleza kwamba uwazi na kasi katika kukabiliana na virusi vya ugonjwa huo hatari ni muhimu katika kudhibiti mlipuko ambao tayari umetajwa kuwa janga la afya duniani.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa Jumamosi, WHO imeeleza kwamba kufuatia taarifa zisizokuwa rasmi kuhusu visa vya ugonjwa na jitihada zake kupata taarifa kutoka kwa idara husika Tanzania kuhusu hali nchini humo, mpaka sasa hawajapokea data za kliniki, matokeo ya uchunguzi, mawasiliano na watu husika na hata matokeo ya uchunguzi wa maabara waliofanyiwa wagonjwa hao wanaoshukiwa.
WHO lilituma kundi la wataalamu kuchunguza kisa cha ugonjwa usiojulikana na ubalozi wa Marekani ulifuatilia hatua hiyo kwa kutoa tahadhari.
Hatua hiyo ilisababisha uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba ugonjwa huo hatari umeingia nchini Tanzania.
Serikali ya Tanzania ilifutilia mbali uvumi kwamba kuna visa vya ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Waziri wa afya nchini humo bi Ummy Mwalimu aliwaambia wanahabari Septemba 14 kwamba hakuna kisa hata kimoja cha ebola katika taifa hilo.
Alisema kwamba taifa hilo limejiandaa kukabiliana na mlipuko wowote wa ugonjwa na tayari limefanya majarabio ili kujua jinsi ilivyojiandaa huku ikiweka tayari vituo vya kuwatenga waathiriwa.