Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:29 am

NEWS: SEREKALI NCHINI ZIMBABWE IMEWAFUTA KAZI ZAIDI YA MADAKTARI 200

Harare: Serikali nchini Zimbabwe imewafuta kazi zaidi ya madaktari 200 kwa kosa la kufanya mgomo wa kudai malipo mazuri ya mishahara.

Taarifa kutoka Harare zinadai kuwa madaktari 211 wamefukuzwa kazi jana ijumaa kwa sababu ya mgomo unaondelea.

Related image

Chama cha madaktari wa hospitali nchini Zimbabwe hakijasema chochote kuhusu taarifa hizi mpya, lakini awali walilalamikia vitendo vya vitisho, shirika la habari Reuters limeripoti.

Madaktari walikutwa na hatia ya kutokuwepo kazini bila likizo wala sababu muhimu'' kwa siku tano zaidi kw mujibu wa taarifa ya Bodi ya huduma za afya (HSB)

Mgomo ulianza mwezi Septemba.

Image result for zimbabwe doctors strike

Bodi hiyo imesema karibu theluthi tatu ya madaktari wote yaani madaktari 516 kati ya 1,601 walioajiriwa kwenye hospitali za serikali wamechukuliwa au watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Mgomo huo umesababisha kuzorota kwa huduma katika hospitali kubwa, ni huduma za dharura pekee ndizo zinazotolewa.

erikali imesema haiwezi kugharamia ongezeko la mishahara wakati ambao raia wa Zimbabwe wanahitaji suluhu ya haraka ya kuondokana na kile wanachokiita mauaji ya taratibu ya kimbari, ameeleza mwandishi wa BBC mjini Harare, Shingai Nyoka.

Zimbabwe iko kwenye hali mbaya kiuchumi na gharama za maisha ziko juu kiasi cha kuathiri vipato vya watu.

Mshahara wa daktari unakadiriwa kuwa kiasi cha pauni 80 kwa mwezi.