Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 6:27 pm

NEWS: SEREKALI KUWACHUNGUZA POLISI WANAOJIHUSISHA BIASHARA DAWA ZA KULEVYA

Naibu Wazari wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Yussuf Masauni amesea Serekali imepanga kuunda tume ya kuchunguza askari wasio waadilifu ambao wanadaiwa kujihusisha na kuomba na kupokea rushwa kama njia ya kupitisha dawa za kulevya katika Visiwa vyua Unguja na Pemba.

Kauli hiyo ya Masauni ameitoa juzi alipozungumza na waandishi wa habari kutokana na kuwapo ongezeko la uingizwaji dawa za kulevya visiwani hapa.

Alisema serikali haijaridhishwa na kasi ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya inayochukuliwa na polisi Zanzibar.

Alisema ongezeko la uingizaji wa dawa za kulevya linatokana na baadhi ya askari wasio waaminifu kupokea rushwa na kuridhia kuingizwa kwa dawa ya kulevya hali inayosababiusha kuwapa mwanya wafanyabiashara wa dawa za kulevya kuendelea kuingiza biashara hiyo.

Alisema tume hiyo itakapokuja itachukua vielelezo vilivyopo kupata urahisi wa kuwatambua askari hao kwa lengo la kuwachukulia hatua za sheria.

“Tunataka tupate mtandao wote wa askari wanaochukua rushwa, hatuwezi kumvumilia askari anayeruhusu kuingizwa dawa za kulevya visiwani mwetu,” alisema Masauni.

Alisema hatua ya kuchukizwa na watendaji wasio waaminifu kwa kuendelea kuruhusu kuingizwa dawa za kulevya hali inayosababisha kuharibika vijana wanaotumia dawa za kulevya na hivyo kupoteza mwelekeo wao wa maisha.

“Hili jambo linaniumiza rohoni kuona vijana wetu wanapoteza mwelekeo wao kwa kutumia dawa za kulevya,” alisema Masauni.

Alisisitiza kuwa jeshi hilo halitawavumilia askari ambao hawatekelezi wajibu wao ipasavyo na kuipeleka Zanzibar kuwa chaka la kuingiza dawa za kulevya.

“Hatuwezi kuendelea kukaa na askari ambao hawafanyi wajibu wao tukastahamili tu.

“Hadi leo kisiwa chetu kinashindwa kudhibiti dawa za kulevya tunatumia mwamvuli wa kujificha kupambana na dawa za kulevya kwa kutumia wahalifu,” alisema.

Chanzo #mtanzania