Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 10:26 pm

NEWS: SEREKALI KUTORUHUSU NDEGE ILIYOSHIKWA KURUDI AFRIKA KUSINI

Serikali imesema haitoiruhusu tena ndege yake ya Airbus A220-300 iliyozuiwa nchini Afrika Kusini kuendelea kufanya safari katika ardhi ya nchi hiyo hadi pale Serikali ya Afrika Kusini itakapoihakikishia usalama wake wa kutua na kuruka bila kukamatwa.

Kauli hiyo imetolewa leo Septemba 5, 2019 na Waziri mwenye dhamana ya uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema wakati wakishughulikia fidia juu ya kesi hiyo ambayo wanasheria wa Tanzania wameshinda, abiria waliokuwa katika route hiyo wataendelea kusafirishwa na ndege zingine hadi hali itakapokuwa shwari.

Kamwelwe amesema kwa mujibu wa ratiba ndege ya Air Tanzania ilitakiwa kwenda Afrika Kusini lakini kutokana na hali ya usalama nchini humo kutokuwa nzuri, safari zinasitishwa kwa muda.

“Tutasitisha kwa muda usafiri wa ndege hadi Serikali itakapofanya mawasiliano na nchi hiyo kwa maandishi kuhakikisha usalama wa abiria na chombo chetu. Hatuwezi kuwapeleka abiria kwenye nchi yenye fujo. Tutawapa taarifa hali itakapotulia,” amesema Kamwelwe.

Ndege hiyo ilizuiliwa katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo nchini Afrika ya Kusini Agosti 23, 2019 kwa amri ya mahakama baada ya Hermanus Steyn kufungua kesi akidai fidia ya dola 33 milioni