- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI KUANZA KUGAWA BURE MAFUTA YA UALIBINO
Dar es salaam: Makama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluh Hassani amesema watu wenye ualbino wataanza kupatiwa mafuta ya kuzuia miale ya jua bure, kutoka katika hospitali za mkoa na wilaya kote nchini.
Akizungumza leo Machi 17 katika hafla ya utoaji tuzo za ‘I CAN’ zilizoandaliwa Taasisi ya Dk Reginald Mengi kwa watu wenye ulemavu, Samia amesema hiyo ni hatua kwa Serikali kuhakikisha huduma za afya kwa watu wenye ulemavu wakiwemo watu wenye ualbino zinaimarishwa.
Mama Samia amezitaka hospitali hizo kuhakikisha wanapoagiza dawa na vifaa tiba kutoka Bohari ya Dawa (MSD), wanaagiza mafuta ya kinga ya ngozi kuzuia miale ya jua ‘sun screen lotion’ kwa ajili ya watu wenye ualbino.
Amesema kutokana na kuwepo kwa saratani ya ngozi inayowakabili watu wenye ualbino nchini, huduma hiyo itaanza kutolewa ili kuwakinga dhidi ya saratani hiyo. “Serikali imetoa maelekezo kwa hospitali zote za Serikali ngazi ya mkoa na wilaya wanapoagiza vifaa tiba kutoka bohari ya dawa (MSD) wameelekezwa kuagiza mafuta ya kinga ya ngozi ya kuzuia miale ya jua (sun screen lotion) yanayotolewa kwa watu wenye ualbino bila malipo,” amesisitiza.
Amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendelea kutoa huduma ya upimaji wa ngozi, macho na matibabu ya saratani katika hospitali za Serikali za Ocean Road, KCMC Moshi, pamoja na Muhimbili.