Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:07 am

NEWS: SEREKALI KUAJIRI WATUMISHI WAPYA 44 811

Dodoma. Serikali ya Tanzania imeahidi kuajiri watumishi wapya wapatao 44,811 katika mwaka wa fedha ujao 2020/2021.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika ameyasema hayo jana Jumatano Aprili 15, 2020 wakati akiwasilisha bajeti yake kwa mwaka huo wa fedha.

Ametaja ajira hizo mpya kuwa ni kada ya elimu (13,529), afya (10,467), kilimo, mifugo na uvuvi (2,145) Jeshi la Polisi (2,725), magereza (685), Jeshi la zimamoto (501), uhamiaji (495) na hospitali za mashirika ya kidini na hiyari (1,262).

Aidha, amesema Serikali inatarajia kuajiri watumishi 13,002 wa kada nyingine zikiwamo za wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma nchini.

Mkuchika amesema pia Serikali itawapandisha vyeo watumishi 222,290 wa kada mbalimbali kulingana na maelekezo yatakayotolewa