November 26, 2024, 7:27 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI IMEWAFUTIA MASHTAKA WAFUNGWA 322 MAGEREZA 7 YA MWANZA
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DDP) Biswalo Mganga, amewafutia kesi askari Polisi nane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba moja ya mwaka 2019 iliokuwa imefunguliwa katika Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Mwanza.
Biswalo alisema pamoja na kuwafutia askari hao kesi hiyo pia amefuta kesi nyingine 322 katika magereza saba ya mikoa ya kanda ya ziwa kwa maslahi mapana ya umma.
DPP ametangaza uamuzi huo jijini Mwanza, mara baada ya kukamilisha ziara yao ya kutembelea mahakama za mikoa hiyo, ambapo waliambatana na Waziri wa Sheria na Katiba, Balozi Agustino Mahiga na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Biswalo alisema kuwa serikali imeamua kufuta kesi hizo 323 ikiwemo ya Askari Polisi hao waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa maslahi mapana ya umma na kwamba serikali imeona hakuna sababu na umuhimu wa kuendelea na kesi hizo.