Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:47 am

NEWS: SEREKALI IMETANGAZA KURUDISHA KODI KWENYE PEDI ZA KIKE

Wiziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza kurujesha kodi kwa waingizaji na wasambazaji taulo za kike endapo hawatashusha bei.

Serekali imeseama wauzaji na wasambazaji wa taulo hizo wameshindwa kupunguza bei kwenye taulo hizo itakayomsaidia mwanafunzi kumudu gharama.

Kauli hiyo imetolewa leo Februari 15, na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa kupinga mimba za utotoni uliyoandaliwa na Taasisi ya Girls Inspire kutoka nchini Canada kwa kushirikiana na Australia, ambao umewakutanisha wadau mbalimbali wa elimu.

Amesema tayari amemwandikia barua Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, kuanza kushirikiana kusimamia suala hilo ikiwa ni pamoja na kupunguza gharama na kuongeza idadi ya taulo hizo badala kuweka sita au nne waweke nane au 10.

“Tuliwapunguzia kodi waingizaji na watengenezaji wa taulo hizo kuhakikisha wanashusha gharama, bei haijapungua kabisa hivyo inabidi tuirudishe maana haijaleta tija kwa watanzania hasa watoto waliopo vijijini ambao hawana uwezo wa kununua taulo hizo kwa kiasi cha Sh 2,000 jambo ambalo hatutalivumilia ,” amesema Waziri Ummy.

Amesema takwimu zilizopatikana baada ya utafiti uliofanywa na Serikali mwaka 2015/16 zinaonesha kati ya watoto wa kike 100 kati yao 27 wamepata mimba wakiwa na umri chini ya miaka 18 ambapo licha ya watoto hao kupata mimba lakini pia wamesababishiwa matatizo mbalimbali ya kiafya.

Amesema madhara ya ndoa na mimba za utotoni nchini ni makubwa kwani licha ya mtoto wa kike kupata matatizo ya kiafya pia husababisha kundi hilo kukosa elimu na hatimaye kuwa maskini kwa kushindwa kutimiza ndoto walizojiwekea.

Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa serikali imejitahidi kuchukua hatua mbalimbali kudhibiti hayo yasiendelee ikiwa ni pamoja na kuanzisha sera ya elimu bure iliyoongeza fursa za watoto wa kike na kiume kupata elimu za msingi na sekondari.

Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole nasha amesema ndoa na mimba za utotoni zinamfanya mtoto wa kike ashindwe kusonga mbele hivyo serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha watoto wa kike wanabaki shuleni na kutimiza ndoto zao