- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SEREKALI IMEKUBALI SHIRIKA LA NDEGE ATCL KUDAIWA SH MILIONI 241
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye amesema serikali inalikumbuka na kulitambua deni la Sh milioni 241 ambalo Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inadaiwa na Mamlaka ya Viwanja vye Ndege Zanzibar na kuahidi kulilipa deni hiyo.
Nditiye ameyasema hayo wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua ni lini serikali italipa deni hilo ambalo ATCL imekuwa ikidaiwa tangu mwaka 2007. “Ni kweli tunakumbuka na kutambua deni la ada ya utuaji ambayo ATCL inadaiwa, deni hilo litalipwa baada ya mamlaka ya ukaguzi ikikamilisha uhakiki, ATCL ilikuwa na madeni mengi ambayo imekuwa ikiendelea kulipa baada ya kufanyiwa uhakiki,” amesema.
Aidha kabla ya swali lake la msingi, Jaku aliipongeza hatua ya serikali hususani Rais John Magufuli ya kufuta VAT kwenye umeme kwa Zanzibar. “Tunapongeza hatua ya serikali kufuta VAT kwa Zanzibar kwenye suala la umeme na hatimaye Zanzibar kupata pumzi baada ya kuwa ICU kwa muda mrefu,” alisema. Katika swali la msingi Jaku alitaka kujua ni kwa nini ATCL kila Jumatatu inapoondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma isipitie Zanzibar ili viongozi pamoja na wananchi wanaotaka kwenda Dodoma wapate huduma hiyo.
Pia aliuliza, Je, Serikali haioni kuwa sasa ni wakati muafaka wa safari za ATCL kutoka Dar es Salaam zipitie Zanzibar kwa Jumatatu zote kupunguza tatizo la usari kwa wananchi wa Zanzibar wanaotaka kwenda Dodoma kwa shughuli mbalimbali.
Jaku pia aliuliza ni lini safari hizo zitaanza ili viongozi, wananchi na watalii kutoka Zanzibar waone kuwa serikali yao inawajali na inadumisha Muungano. Akijibu maswali ya nyongeza, Waziri Mditiye alisema dhumuni la serikali kupitia ATCL ni kuhakikisha wananchi wote wa bara na visiwani wanapata huduma ya usari wa anga kwenye kituo chochote chenye maslahi ya biashara. “Hata hivyo, ATCL inatumia kituo cha Dar es Salaam kama kitovu ili kuwa na muungano wa kupeleka abiria sehemu nyingi na kukidhi mizania ya kibiashara,” alisema.
Alisema baada ya kubaini Zanzibar kuwa ni moja ya vituo ambavyo kuna maslahi ya biashara, imerekebisha ratiba ili kuhakikisha wasari kutoka Zanzibar wanakuwa na uwezo wa kusari kwenda Dodoma kupitia Dar es Salaam kwa kuwa na ndege siku ya Ijumaa na Jumapili. Nditiye pia alisema utaratibu wa safari za ATCL kutoka Dar es Salaam kupitia Zanizbar kwa kila Jumatatu utaanza pindi muunganiko wa kupeleka abiria Zanzibar kutoka Dar es Salaam na sehemu zingine kwa siku ya Jumatatu utakapokidhi mizania ya kibiashara. “Serikali inawajali viongozi, wananchi na watalii kutoka Zanzibar na ndiyo maana inajitahidi kwa kila hali kuhakikisha kuwa viongozi wananchi na watalii kutoka Zanzibar wanapata usari wa kuunganisha kutoka kituo cha Dar es Salaam kama kitovu kwenda Dodoma kwa kadiri inavyowezekana,” amesema.