- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SAYONA YAMFADHILI HARMONIZE
Dar es Salaam. Msanii Rajab Abdul maarufu Harmonize amesema makubaliano mapya na kampuni ya Sayona ndio sababu ya mgahawa wa ‘Konde Boy’ uliopo katika gari kutoonekana mtaani.
Kupitia mgahawa huo uliozinduliwa Oktoba 20, 2019, msanii huyo anayetamba na wimbo Uno na Kainama hugawa chakula mitaani kinachokuwa kimefungashwa katika mifuko midogo iliyoandikwa ‘Konde Boy mgahawa’.
Gari hilo lilipangwa kupita mitaani kila Jumapili kugawa chakula na siku ya uzinduzi ziliibuka vurugu kutokana na waliojitokeza kusukumana, kila mmoja akitaka kupata chakula.
Akizungumza leo Jumatano Januari 15, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari, Harmonize amesema sababu ya gari hilo kutoonekana mtaani ni makubaliano aliyoingia na Sayona.
Msanii huyo ambaye leo ametangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Twist amesema ugawaji wa chakula hicho ulifanyika kwa takribani wiki tano, baadaye kusitishwa baada ya kampuni ya Sayona kuomba kuwaunga mkono