Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 4:50 pm

NEWS: SAUDIA YARUHUSU WAPENZI KULALA CHUMBA KIMOJA

Tokeo la picha la saudi arbia rooms

Taifa la kifalme Saud Arabia limeruhusu Wapenzi raia wa kigeni ambao hawajaoana sasa wanaweza kulala chumba kimoja na kufurahia maisha.

Tokeo la picha la saudi arbia rooms

Hatua hiyo imekuja mara baada ya kufanya mabadiliko ya masharti ya kupata viza yaliyotangazwa hivi karibuni na taifa hilo ambalo limekuwa likiendeshwa na sheria za kihafidhina za dini ya Kiislamu.

Pia Wanawake pia sasa wataruhusiwa kupanga vyumba vya hoteli peke yao.

Wapenzi hapo awali walitakiwa kutoa uthipitisho wa kuwa wameoana kabla ya kupata chumba cha hoteli.

Mabadiliko hayo yanakuja katika kipindi ambacho serikali ya Saudia inajipanga kukuza sekta ya utalii nchini humo.

"Raia wote wa Saudia wanatakiwa kuonesha vitambulisho vya familia ama uthibitisho wa mahusiano wakati wa kukodi vyumba vya hoteli," ameeleza Kamishna wa Utalii na Urithi wa Taifa wa Saudia katika taarifa yake.

"Uthibitisho huo hata hivyo hautawahusu watalii raia wa kigeni. Wanawake wote, wakiwemo raia wa Saudia sasa ruksa wanaweza kupanga vyumba vya hoteli wakiwa peke yao, alimradi tu wawe na vitambulisho."

Mwanamfalme Mohammed bin Salman katika miaka ya hivi karibuni amejaribu kufanya mabadiliko katika nchi hiyo ambayo viongozi wa kidini wa kihafidhina ndio wamekuwa wakiamua nini kiwe sheria.

Mabadiliko hayo yamehusisha kuondolewa kwa marufuku ya wanawake kundesha magari, na kuwaruhusu wanawake kusafiri bila ya kusindikizwa ama kupata ruhusa ya mwanaume.

Hata hivyo mabadiliko yote hayo yamemezwa na mambo mengine yanayoendelea nchini humo ikiwemo mauaji ya mwanahabari Jamal Khashoggi.

Simon Calder, ambaye ni mhariri mwandamizi wa habari za utalii na safari wa gazeti la The Independent, amesema kulegeza masharti ya viza kutaleta ongezeko kubwa la watalii nchini humo.