Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 2:43 pm

NEWS: SAUDIA YAFUTA SAFARI ZA KUHIJI MAKKA

Serikali ya nchini Saudi Arabia imezuia wageni wote wanaoingia nchini humo kwa safari za kidini, zikiwemo safari za wanaotembelea miji mitakatifu ya Makka na Madina kwa ajili kufanya maombi ya kidini kwa kuhofia ugonjwa wa Corona Virus.

Watu duniani kote huingia Saudia mwaka mzima kufanya ibada ya Umra, na wengi zaidi huingia kwa pamoja kufanya ibada ya Hija.

Tofauti na Hija, Umra hufanyika katika kipindi chochote cha mwaka, na kwa sasa marufuku hiyo inawalenga mahujaji raia wa nchi za nje wanaoenda kuitekeleza.

Bado haijulikani kama ibada ya Hija, ambayo inategemewa kuanza mwishoni mwa mwezi Julai kama itaathirika na zuio hilo pamoja na kusambaa kwa virusi vya corona duniani.

Saudia pia imewapiga marufuku watu kutoka nchi zilizokumbwa na virusi hivyo kuingia nchini humo.