- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
News: Samia Suluhu anatarajiwa kufungua mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya ujenzi
Dodoma: MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufungua mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya ujenzi ambao unatarajiwa kuwakutanisha zaidi ya wakandarasi 1,000 wa ndani ya nje ya nchi.
Ameyasema hayo bungeni mjijini dodoma na Msajili wa Bodi ya Wakandarasi (CRB), Rhoben Nkori, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo wa siku mbili utakaofanyika mkoani Dodoma.
Nmakori amesema kaulimbiu ya mwaka huu ni “Miaka 20 ya CRB; Uwajibikaji uliotukuka kwa Wakakandarasi kama njia ya kuwavutia wateja” Good Conduct and Compliance as a Strategy to Win Clients’ Trust”.
Samia amesema dhumuni la mkutano huo ni kuwakutanisha kwa pamoja wadau wa sekta nzima ya ujenzi ambapo watajadili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo na kuweka mikakati ya pamoja ya namna wanavyopaswa kutekeleza miradi kwa namna ambayo itawaridhisha wateja wao na kuonyesha uaminifu kwao.
“Wakandarasi wote wanatakiwa kushiriki kwa kuzingatia kuwa wale watakaoshiriki watahesabika kuwa wamepata alama za CPD ambazo hutumika kwaajili kukuza wasifu wa makampuni yao. Bodi inawataka wamiliki, wadau, wakurugenzi ambao ni wafanyamaamuzi kwenye makampuni yao kushiriki bila kukosa kwasababu maazimio yatakayotokana na mkutano huo yatakuwa na msaada mkubwa kwenye sekta ya ujenzi kwa jumla,” alisisitiza.
Amesema mkutano huu utawaleta pamoja wakandarasi, washauri, wateja wa kazi za wakandarasi, watunga sera, wadhibiti, (Regulators) na wadau wengine wa sekta ya ujenzi ambao watajadiliana na kutoka na maazimio mbalimbali kuhusu changamoto zinazoikabili sekta ya ujenzi nchini na nini kifanyike kuboresha kazi za wakandarasi wazalendo.
“Kutakuwa na mada mbalimbali zitakazowasilishwa na bodi ya CRB, Wateja, Wadhibiti, wadau wa viwanda na wadau wa taasisi za kifedha ambao washiriki wa mkutano huo kwenye mijadala inayohusiana na fedha na mikopo…..Jumla ya mada saba zitawasilishwa kuhusu mafanikio ya sekta nzima ya ujenzio na namna ya kuboresha shughuli za wakandarasi na namna ya kukidhi vigezo vilivyowekwa,” amesema.