- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SALOME MAKAMBA AHOJI SAKATA LA UHABA WA MAJI KATIKA MJI MZIMA WA SHINYANGA
Dodoma: MBUNGE wa Viti Maalum, Salome Makamba (Chadema) ameitaka Serikali ieleze ni kwanini kwa sasa miji wa shinyanga na Kahama hawajapata maji kwa muda wa wiki mbili na hawajalipa bili ya umeme kama alivyoagiza rais wa Tanzania John Magufuli.
Salome amehoji wakati wa kipindi cha maswali na majibu alipokuwa akiuliza swali la nyonyeza kwa kutaka kujua ni lini maji yatarejeshwa kati miji ya Shinyanga na Kahama na lini watalipa bili ya Umeme kama alivyo agiza rais John Mafufuli.
Awali katika swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum, Aziza Hamadi(CCM) alitaka kujua ni lini serikali itakamilisha ahadi ya kuchimba bwawa la mradi wa umwagiliaji Masengwa katika wilaya ya halmashauri ya Shinyanga.
Akijibu swali la nyongeza la Makamba Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe amesema kuwa ni kweli halmashauri hiyo haina maji kwa wiki moja au mbili kwa sasa.
Amesema tatizo hilo linatokana na mamlaka kushindwa kulipa bili za Umeme jambo ambalo kwa sasa limechukuliwa kwa umakini ili kuhakikisha maji yanalipwa ili wanannchi wapate huduma ya maji.
Akijibu swali la msingi Kamwelwe, alisema skimu ya umwagiliaji ya Masengwa ambayo ilijengwa katika mwaka 2004 na 2006,chini ya programu shirikishi ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ina eneo lililoboreshwa lipatalo hekta 325.
Hata hivyo eneo linalolimwa linafikia hekta 800,aidha kutokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi imeshuhudia ukame hali ambayo imewafanya wakulima wawe na hitaji la kujengewa bwawa kwa ajili ya kutunza maji