- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SAKATA LA MCHANGA WA DHAHABU WAMPONZA MNYIKA
DODOMA: SAKATA la Mchanga wa dhahabu limeingia katika sura mpya kwa wabunge kurushiana vijembe vya hapa na pale Bungeni hali iliyosababisha Mbunge wa Kibamba John Mnyika (Chadema) kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya Bunge kwa wiki nzima ijayo kwa kile kilichodaiwa ni kudharau kiti cha spika.
Leo Mnyika ametolewa ndani ya ukumbi wa Bunge kwa kubebwa juu juu na Askari wa Bunge mpaka nje ya viwanja vya Bunge kwa amri ya Spika wa Bunge Job Ndugai.
Mbali na Mnyika kupewa adhabu hiyo,Spika Ndugai pia ameagiza Kamati ya Maadili,Kinga na Madaraka ya Bunge kukutana Jana mchana ili iweze kumuita Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya (Chadema) ambaye pia ni kaimu Mnadhimu wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni pamoja na Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) kutokana na vurugu walizozionesha baada ya Mnyika kutolewa Bungeni.
"Lakini wakati vurugu zikitokea mmemuona Bulaya alivyokuwa analeta fujo,nataka Kamati ya maadili mchana huu mkutane ili Mheshimiwa aitwe Leo hii na apewe samansi ili asije akatoroka Dodoma ,na hata Kama hatakuwepo lazima kikao kifanyike kesho na jumatatu tunaanza na hukumu hiyo.
"Pia , wakati Askari wanamtoa Mnyika ,Mdee alikuja akavamia Askari akawa anavuta koti la Askari ili kumchania koti lake,ni jambo la aibu kwa Mbunge kulifanya,tunaikumbushia Kamati ya maadili adhabu yake,na jumatatu naye tunaanza naye." amesema Spika Ndugai
Hatua ya kuwapa adhabu ya wabunge hao imefikiwa na Ndugai baada ya Mnyika kubishana na kiti cha Spika wakati Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde (CCM) akichangia bajeti ya Nishati na Madini (iliyohitimishwa Leo ).
Akizungumza wakati akiahirisha Bunge jana saa saba mchana ,Ndugai amesema,tangu Mnyika alipoanza kusimama kuomba utaratibu,amekuwa akisimama na kuzungumza bila kufuata kanuni yoyote ile ya Bunge lakini amekuwa akimruhusu.
"Toka mwanzo sikutaka kumbana kikanuni kwa kuwa alikuwa nje ya kanuni,alikuwa analeta fujo ,kubishana na Spika kwa kiwango kisichoweza kuvumilika,kwa hiyo nimempa adhabu hiyo ,tumesikia anasema atakata rufaa,tunamsubiri kwa ujuaji huo." amesema Ndugai
Mapema kabla ya Lusinde kuanza kuchangia,Mnyika akichangia katika wizara hiyo aliitaka Serikali kuangalia mikataba ya Madini badala ya kung'ang'ania mchanga ambao una Madini kidogo.
Sakata lilivyoanza
Wakati Lusinde akichangia,alizungumzia sakata la mchanga wa Dhahabu uliozuiliwa na Rais John Magufuli ambapo aliwashangaa wapinzani kwa kuwatetea aliowaita wezi wa Madini nchini.
Hali hiyo ilimfanya Mnyika kuomba ruhusa ya Spika ili ampe taarifa Lusinde ambapo alipopata taarifa alisema,Lusinde amepotosha na kwamba hakuna mpinzani yeyote anayetetea wizi wa dhahabu katika mchanga wa makinikia.
Lakini wakati Spika anamwita Lusinde kumhoji kuhusu kuipokea taarifa hiyo,Mnyika amedai kuna Mbunge aliwasha kipaza sauti na kusema 'Mnyika mwizi' hali iliyomfanya Mnyika kumwomba Spika Mbunge aliyetamka maneno hayo ayafute kwa sababu yeye siyo mwizi.
Hata hivyo Spika alimsihi Mnyika akae chini ili mzunguzaji aliyekuwa akichangia ,aendelee kutoa mchango wake lakini mara kadhaa kila mzungumzaji alipoanza kuzungumza,Mnyika naye alisimama na kuzungumza kinyume cha kanuni za Bunge ndipo Ndugai alipoamuru Askari wa Bunge wamtoe Mnyika mpaka nje ya viwanja vya Bunge lakini pia asihudhurie vikao vinavyofuata kwa wiki nzima.
Hatua ya Mnyika kutolewa nje ya Bunge,Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya (Chadema) ambaye amekaimu nafasi ya Mnadhimu wa kambi ya Upinzani Bungeni,aliwaamuru wabunge wote wa Upinzani watoke nje ya Bunge kama sehemu ya kutoridhishwa na maamuzi ya kiti.
Nje ya ukumbi wa Bunge
Kaimu Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Bulaya akizungumza na waandishi wa habari amesema,kambi haikuridhishwa na Spika kuamua kuendelea kuzungumza lugha mbaya na kuamua cha mtu aliyewahi kuanza sauti na kusema Mnyika mwizi.
Spika alipaswa kutumia busara ya kumtaka aliyemwita Mnyika mwizi afute kauli yake au atoe maelekezo ichunguzwe ni nani amesema ili apelekewe kwenye Kamati ya maadili lakini haikuwa hivyo
Anasikitishwa kuona sasa hivi CCM wanashangilia mchanga wakati Upinzani ndio walikuwa we kwanza kulipigia kelele suala hilo,lakini imekuwa kawaida kiti cha Spika kuwaonea wabunge wa Upinzani hali aliyosema,wao hawawezi kukubaliana na uonevu huo.
Kwa upande wake Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) alisema,kwenye Kamati ya maadili ataenda ingawa anajua anaenda kushughulikiwa kwa kuwa wanajua mkakati wa Serikali kwa wabunge wa Upinzani.
"Hakuna Siku ambayo Serikali inaweza kuwa kitu kimoja na Upinzani na badala yake kila Siku wamekuwa wakitupinga na kutuonea." alisema Mdee
Alisema,kwa kutika nje ni kuonesha kwamba kambi hiyo haijaridhika na maamuzi huku akisema,Spima a lipaswa kutumia busara ya kufuatialia taarifa katika kumbukumbu za Bunge (Hansard) kwa ajili ya hatua zaidi Kama inavyofanyika kwa wabunge wengine akiwemo yeye.
Hata hivyo alisema,katika suala la Madini na rasilimali nchini,Upinzani wamekuwa wakizungumza kwa muda mrefu na kwamba hakuna hata Siku moja ambayo wabunge wa CCM wamewahi kuzungumzia hilo .
Amesema,cha kusahangaza,ghafla wao ndio wamekuwa na uchungu na suala la Madini eti kwa sababu Rais Magufuli amezuia makontena ya mchanga kusafirishwa nje ya nchi kwa uchunguzi.
"Lakini sisi tumesema mchanga ni kiduchu Kati ya vitu vingi,Bunge lijadili ili tuazimie tupate mikataba yote ya Madini,Sheria za Madini ambazo zinalinda maslahi ya wawekezaji ambazo zimebinafsisha ,tunavyozungumza Madini ni ya watu binafsi ,Serikali inapata kashea ketu kidogo kwa asilimia nne kutokana na mikataba na Sheria zinavyosema,
"Sasa tunasema hiyo isiwe ajenda kubwa,bali kama Bunge ajenda ambayo tunatakiwa kuishauri Serikali ,mikataba na Sheria zote za Madini iletwe Bungeni ,tuangalie wapi tumeteleza kwa kadri ambavyo wataalam wanashauri,lakini hawataki kusikia." amesema Mdee