Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 6:43 pm

NEWS: SAKATA LA CAG LAWAGOMBANISHA ZITTO NA MSEMAJI WA SEREKALI

Sakata la Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serekali (CAG) Prof. Mussa Assad limeendelea kuwa kaa la moto kwa viongozi wa serekali, wanasiasa na Wananchi baada ya leo asubuhi sakata hilo kumuibua Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe aliyedai kuwa magazeti takribani yoote yaliyoandika Uchambuzi wa ripoti ya CAG ya Chama cha ACT Wazalendo chini ya Kiongozi wake huyo wamelimwa barua ya kutakiwa kujieleza na Msemaji mkuu wa serekali DktHassan Abbas

"Msemaji mkuu wa Serekali kaandikia barua magazeti yote, yaliyoandika habari ya uchambuzi wa Ripoti ya CAG uliofanywa na ACT Wazalendo. amewataka wajieleze kwa kuvunja sheria. Sasa msemaji wa serekali amekuwa Mhariri wa Taifa" aliandika zitto kwenye ukurasa wake wa Twitter

April 14, 2019 Kiongozi Mkuu huyo wa ACT Wazalendo kwa niaba ya chama chake aliwasilisha kwa wanahabari uchambuzi wao wa ripoti ya CAG na akainisha maeneo 10 muhimu kwenye Ripoti ile ya CAG . Baadhi ya uchambuzi wake ulionesha hivi :

1. Bajeti ya Serikali Sio Halisia, Mapato Yasiyokusanywa ni Tarakimu Mbili.

2. Asilimia 40% ya Bajeti Inategemea Misaada na Mikopo

3. Shilingi 800 Bilioni Hazikutolewa kwa Ukaguzi

4. Shilingi 4.8 Trilioni Zimetumika Bila Kupita Kwenye Mfuko Mkuu

5. Bilioni 678 za Mamlaka Nyengine Ziliporwa na Mlipaji Mkuu wa Serikali

Baada ya Madai hayo ya Zitto Msemaji mkuu wa Serekali Hassan Abas Imemlazimu kumjibu mbunge huyo kwa kukiri kuwaandikia barua na kusema kuwa wenyewe walioandikiwa Barua hizo wamekiri kosa lao na kwanini vyombo hivyo vimempa taarifa Zitto ya juu ya kuandikiwa barua.

"Zitto Kabwe Kama hili ni andiko lako pokea/puuzia ushauri: 1.Usilete siasa ktk taaluma ambayo bahati mbaya huijui misingi yake.Walioandikiwa wamejua/kukiri kosa lao. 2.Kama waliandikiwa, wakaripoti kwako sasa tumejua wewe ndie MhaririMkuu unaewapotosha kila siku. Acha" alisema Dkt Abas