Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:02 am

NEWS: SAFU YA TAKUKURU KINONDONI YAPANGWA UPYA

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania, Brigedia Jenerali, John Mbungo amepangua safu ya uongozi wa taasisi hiyo Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Muakilishi TZ Twitter પર: "#MuakilishiNews Kaimu Mkurugenzi Mkuu ...

Brigedia Jenerali, Mbungo amesema leo Jumatatu tarehe 11 Mei 2020 amefanya uamuzi huo baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi juu ya watendaji wake kutokutimiza wajibu wake ipasavyo.

Kwa nyakati tofauti mwezi Machi 2020, Takukuru iliwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wake wa Kinondoni na Tanga wakiongozwa na mabosi wa maeneo hayo kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Kigogo anaswa na TAKUKURU | East Africa Television

Tarehe 20 Machi 2020, Brigedia Jenerali Bungo aliwasimamisha kazi watumishi wawili ambao ni mkuu wa taasisi hiyo mkoani Tanga, Christopher Mariba pamoja na Afisa Uchunguzi Mkuu wa Takukuru, Hilton Njauna kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa mmoja wa watuhumiwa waliokuwa wakichunguzwa na taasisi hiyo. Tarehe 26 Machi 2020, Brigedia Jenerali, Mbungo alitangaza kuwasimamisha kazi watumishi watano wa Kinondoni wakiongozwa na Mkuu wa Takukuru Kinondoni, Teddy Mjangira kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yao. Teddy na wenzake wanatuhumiwa kufanya uchunguzi kwa mtu ambaye hakupaswa kuchunguzwa hali iliyosababisha usumbufu kwa mtu huyo.

Brigedia Jenerali Bungo amesema uchunguzi dhidi ya tuhuma zao unaendelea na utakapokamilika watafikishwa mahakamani. Amesema kwa Mkoa wa Takukuru wa Kinondoni, “Tumewatoa maeneo yao ya kazi, Kinondoni nzima ilikuwa haijakaa vizuri. Kulikuwa na malalamiko mengi kuhusu watendaji wa Kinondoni na tumepangua safu nzima kuanzia kiongozi mkuu na tumepeleka sura mpya kabisa.” Kuhusu uchunguzi ulipofikia mkoani Tanga, Brigedia Jenerali Bungo amesema uchunguzi umefikia hatua za mwisho akisema, “uchunghuzi uko tayari kupelekwa mahakamani, kuna mmoja tuna ushahidi wa kutosha kuweza kusimamisha mashtaka mbele.”