- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SAFARICOM YAPATA FAIDA YA KSH BILIONI 35.7 KWA KIPINDI CHA MIEZI 6
KAMPUNI ya mawasilino ya Safaricom imepata faida ya KSh35.65 bilioni baada ya mapato ya M-Pesa na data Kwa kipindi cha miezi sita hadi kufikia Septemba 2019 na kuongezeka kwa asilimia 14.4 licha ya mapato kutokana na kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi (SMS) kupungua.
Huu ni mwaka wa nane sasa ikiendelea kupata faida baada ya kuondoa makato mengine ikiwemo ushuru.
Katika kipindi cha miezi sita, mapato kutokana na M-pesa yalikuwa kwa asilimia 18.2 na kufikia Sh41.97 bilioni nayo ya vifurushi vya data ya Intaneti kuongezeka kwa asilimia nne hadi kuwa Sh19.78 bilioni.
Mapato kutokana na huduma za wateja ama kupiga simu au kupokea ambayo huwa tegemeo kuu la kampuni hiyo yalipungua kwa asilimia 1.4 na kuwa Sh46.87 bilioni nayo yale ya huduma za ujumbe mfupi yalipungua kwa asilimia 11 na kuwa Sh8.6 bilioni.
“Ukuaji wa mapato kipindi cha nusu-mwaka hadi Septemba ulikuwa wa asilimia 5.3 uliochochewa zaidi na huduma za M-Pesa na data pamoja na ukuaji wa wateja na hivyo kusawazisha sehemu za mapato kuporomoka ambazo awali zilikuwa ni tegemeo,” amesema Afisa Mkuu Mtendaji wa Safaricom anayeondoka Michael Joseph akitangaza ripoti hiyo ya kampuni katika makao makuu jijini Nairobi.