- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SADC YAPENDEKEZA KUUNDWA SEREKALI YA MSETO CONGO DRC
Muungano wa maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika SADC, imetoa pendekezo la kuundwa kwa serikali ya muungano nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia mzozo wa kisiasa unaoendelea kutokana na matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi uliyopita 2018.
Taarifa hiyo imetolewa kupitia taarifa ya rais wa Zambia Edgar Lungu.
Afrika Kusini pia inaunga mkono wazo la kubuniwa kwa serikali ya muungano
Mapendekezo hayo ya SADC yanakuja siku moja baada ya mgombea wa upinzani katika uchaguzi mkuu uliyofanyika nchini Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo amewasilisha kesi katika mahakama ya katiba kupinga matokeo ya uchaguzi huo.
Martin Fayulu amesisitiza kuwa alishinda uchaguzi huo lakini tume ya uchaguzi ikamtangaza mshindani wake Felix Tshisekedi kuwa mshindi.
Rais wa Zambia, Edgar Lungu, amesema kuwa wamezingatia "mvutano mkali uliyoibuka" kupinga matokeo ya awali.
Bwana Lungu alitoa mfano wa mwafaka wa kisiasa uliopatikana nchini Zimbabwe na Kenya.
Waziri wa mambo ya nje wa Afrika Kusini,Lindiwe Sisulu, anapendekeza mchakato wa kisheria ufuatwe DRC kuhusiana na suala hilo huku akitoa wito kuwa watu wa nje wasiwalazimishe Wacongo jambo ambalo hawajaridhia.