- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: SABABU ZA KUTIMULIWA KWA MKUU WA UPELEZI (FBI) CHINI MAREKANI
Washington: Rais wa Marekani Bw. Donald Trump Jana juma nne alimtimua kazi Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), Bw. James Comey, hatua ambambyo imepelekekea kuwepo kwa tafrani za kisiasa nchini humo kati ya vyama viwili vyenye nguvu nchini marekani.
Kwa mujibu wa shirika la Habari la The New York Times linasema kuwa Comey ametimuliwa katika nafasi hiyo kwa sababu kuu mbili, Moja ni hatua yake katika namna alivyo shughulikia uchunguzi kuhusiana na barua pepe za aliyekuwa waziri wa mambo ya kigeni na aliye kuwa mgombea wa Urais mwaka jana Hillary Clinton. Pia sababu ya pili ya msingi ni namna Bw. Comey alivyo weka ahadi ya kuendelea na uchunguzi kwenye swala la Urusi kuingilia uchaguzi wa marekani mwaka jana 2016
Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya White House imesema Comey aliachishwa kazi kwa kuzingatia mapendekezo ya wazi kutoka kwa Mwanasheria Mkuu Jeff Sessions na Naibu wake Rod Rosenstein. Rosenstein amekosoa namna Comey alivyoshughulikia kashfa ya barua pepe za Clinton, ikiwa ni pamoja na kukataa mwezi Julai kumfungulia mashitaka na pia matamshi yake ya umma kuhusiana na uchunguzi huo.