Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:51 am

NEWS: RWANDA YAONGEZA MUDA WA MARUFUKU WA KUTOKA NJEE

Serikali ya Kigali imeongeza muda wa siku 15 wa marufuku ya kutotoka nje iliyowekwa mwezi uliopita, mpaka tarehe 19 mwezi Aprili mwaka huu.

Idadi ya watu walioambukizwa na coronavirus nchini Rwanda imefikia watu 75.

Familia zilizoathiriwa na sheria ya kukaa nyumbani , nchini Rwanda zilipokea msaada wa Chakula kutoka kwa serikali ya nchi hiyo.

Kagame cautions against panic as Rwanda confirms first coronavirus ...

Familia hizo ni zile zilizoathiriwa na agizo la kukaa nyumbani liliyowekwa nchini humo ili kukabiliana na maambukizi ya coronavirus.

Rwanada iliweka Marufuku ya kutotoka nje iliyoanza tarehe 21 mwezi Machi iliwazuia watu kuondoka majumbani mwao isipokuwa tu kwenda kununua chakula na dawa.

Serikali imewasambaza askari kwa ajili ya kuhakikisha kuwa marufuku hiyo inatekelezwa ipasavyo.

Marufuku hiyo ilikuwa ikitarajiwa kuisha mwishoni mwa juma hili lakini muda uliongezwa na baraza la Mawaziri baada ya idadi ya walioambukizwa kuongezeka kutoka 17 mpaka 82 kwa majuma mawili.

Wakati huu wa nyongeza ya muda, mipaka itaendelea kufungwa na raia wa Rwanda pekee ndio watakaoruhusiwa kuingia nchini humo.

Mizigo itaendelea kuingizwa nchini Rwanda.

Maduka, shule, maeneo ya kufanya ibada yatafungwa na waajiriwa wataendelea kufanya kazi wakiwa nyumbani, pia vyuo na shule zimetakiwa kutumia teknolojia kuendelea kutoa maelekezo ya masomo.

''Shughuli za kilimo zitaendelea wakati huu wa maandalizi ya msimu wa kilimo huku wakulima wakiamriwa kufuata taratibu na maelekezo kutoka mamlaka za afya'', waraka wa baraza ulieleza.