- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RUWASA KUANZA UTEKELEZAJI WA PROGRAMU MAALUM YA UJENZI WA MIRADI YA MAJI IKAYOHUDUMIA VITUO VYA AFYA.
SINGIDA: Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Prof. Kitila Mkumbo amewataka Mameneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika mikoa yote 26 wabuni programu maalumitakayomaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji katika vituo vya afya ili kuimarisha huduma zinazotolewa katika maeneo hayo.
Prof. Mkumbo ameielekeza RUWASA kuandaa bajeti kwa mwaka ujao wa fedha 2020/21 ili kufanikisha utekelezaji wa programu hiyo mahsusi inayolenga kuimarisha u patikanaji wahuduma ya maji ya uhakika kwenye vituo vyote vya afya nchini, itakayopelekea utoaji wahuduma bora za afya itakayochochea ustawi na maendeleo ya jamii.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Maji na Umeme katika vijiji vitatu vya Mtavira, Mungaa na Makotea katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida uliogharimu kiasi cha Shilingi milioni 861 kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Programu yaMaendeleo (UNDP).
Prof. Mkumbo amesema kumekuwa na malalamiko mengi kwa vituo vya afya kukosa huduma ya maji ya uhakika, jambo ambalo linahatarisha afya za wananchi, ustawi na maendeleo ya taifa kwa ujumla, ikingizatiwa kuwa ni moja ya maeneo muhimu yanayotakiwa kuwa na maji yakutosha muda wote ili viweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
Aidha, ameishukuru sana UNDP kwa kushiriki katika kuleta maendeleo ya Sekta ya Maji nchini na kusaidia kumaliza tatizo la maji katika Wilaya ya Ikungi iliyokuwa na asilimia 41, kiwango chachini kabisa cha upatikanaji wa majisafi na salama kwa wilaya zote mkoani Dodoma.
Meneja Mradi, Emmanuel Nko amesema hatua ya utekelezaji wa mradi huo utakaohudumia wakazi zaidi ya 9,000 imekuja baada ya UNDP kubaini uhaba na uhitaji mkubwa wa maji katika vijiji vya Mtavira, Mungaa na Mkotea na umeongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma yamaji wilayani Ikungi kwa asilimia 4 mpaka kufikia asilimia 45 kwa sasa.
Ujenzi wa mradi huo unaotumia nishati ya jua una jumla ya vituo 18 vya kuchotea maji, ulianza rasmi Juni, 2019 na kukamilika Disemba 13, 2019.
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini