Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 1:57 pm

NEWS: RUSHWA YAMPOZA RAIS WA ZAMANI WA BRAZIL AHUKUMIWA MIAKA 9 JELA

BRAZIL: Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Ignacio Lula da Silva, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa unusu jela miongoni mwa kesi tano za ulaji rushwa zinazomkabili.

Lula aliondoka kutoka umaskini enzi za utoto wake na kuwa mmoja wa marais maarufu zaidi wa Brazil.

Kiongozi huyo wa zamani wa chama cha muungano alijizolea umaarufu kutoka jamii ya kimataifa kwa sera zake za kijamii ambazo zilisaidia kuboresha maisha Brazil.

Image caption Dilma Rousseff aliondolewa madarakani Agosti 31, 2016 kwa kashfa ya rushwa

Lakini sasa mambo yamegeuka na kukutwa na hatia ya kukubali hongo ya zaidi ya dola milioni moja za malipo ya ghorofa ya mapumziko kwa ajili ya ukarabati wake kwa kampuni ya ujenzi ya Ki Brazil, iitwayo kwa kifupi OAS.

Hukumu hii inakuja wakati ambapo mtawala Lula akiwa ametoa msimamo mkali kwamba ana mpango wa kuingia katika kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya urais mwakani .

Kufuatia hukumu hiyo, rais huyo amekana mashtaka yote yanayomkabili kwa kudai kuwa hajafanya makosa yoyote kiasi cha kustahili hukumu hiyo, huku mawakili wanaomtetea wameapa kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Image caption Rais aliyepo Michel Temer anajadiliwa iwapo aondolewe madarakani kwa kashfa hiyo

Wakati huo huo, kamati ya Bunge la Congress ya Brazil inajadili iwapo iiruhusu mahakama kuu kusikiliza kesi ya rushwa inayomhusisha Rais wa Brazil Michel Temer.

Temer alishtakiwa mwezi uliopita kwa tuhuma za kupokea hongo kutoka kampuni kubwa ya usindikaji nyama.

Image caption Waandamanaji wengi wanataka Rais wa sasa Michel Temer kuachia ngazi kutokana na kashfa ya rushwa

Kamati hiyo inatarajiwa kupiga kura hapo kesho.

Iwapo pendekezo hilo litapita, suala hilo litajadiliwa katika bunge dogo la wawakilishi, ambapo theluthi mbili itahitajika kupiga kura ili Rais ashitakiwe.