Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 3:41 am

NEWS: RUSHWA YA NGONO VYUO VIKUU YAIAMSHA SERIKALI.

DODOMA: Wakati vitendo vya ukatili wa kijinsia na rushwa ya ngono vikidaiwa kushamiri katika Vyuo vya elimu ya juu hapa nchini, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii imeibuka na kutangaza mkakati wa kutokomeza tatizo hilo.


Hayo yamebainishwa leo jijini hapa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. John Jingu, wakati akifungua kikao kilichowakutanisha wawakilishi wa vyuo vya elimu ya juu kilichoketi kwa lengo la kuzungumzia namna ya kupambana na ukatili wa kijinsia katika maeneo ya Vyuo vya elimu ya juu.

Dkt. Jingu amesema kuwa katika kuhakikisha vitendo hivyovya ukatili wa kijinsia na rushwa ya ngono vinakomeshwa hapa nchini, Serikali na Wadau wengine watajikita katika kutekeleza mkakati wa kukomesha kwa asimilia 50 hadi ifikapo 2021 na 2022.

“Mpango Mkakati huu unalenga kutokomeza vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia na rushwa ya ngono ifikapo 2022 ili kusudi wanafunzi wa kike wanaosoma elimu ya juu waweze kufanikisha malengo yao bila kuwepo vikwazo kama vya kuombwa rushwa ya ngono” amesisitza Dk. Jingu.


Aidha Dkt. Jingu amewataka wakuu wa vyuo hao kuhakikisha wanatoa elimu na maelekezo ili kujenga uelewa wa kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanafunzi wa kike kwa kwa ajili ya kuepuka matakwa ya wahadhiri wanaotumia hila kuendekeza ukatili wa kingono vyuoni.

Pia Dkt. Jingu amewataka Wakuu wa vyuo hao kuhakikisha wanatekeleza Agizo la Waziri Ummy Mwalimu la kuanzisha madawati ya jinsia katika vyuo vyao ili kuwezesha kuondokana na vitendo vya kikatili na kujenga mazingira yaliyosalama katika vyuo vyetu.

Kwa upande wake Mkuu wa Uelimishaji kutoka Taasisi ya Kupambana na Kutokomeza Rushwa TAKUKURU Bw. Asseri Mandari amesema kuwa Taasisi hiyo imejipanga kupamabana na tatizo hilo kwa kuanzisha Kampeni inayaosema “Vunja Ukimya Ondoa Rushwa ya Ngono” itakayosaidia kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kuzuia rushwa ya ngono.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Jinsia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt. Lulu Mahai amesema kuwa Vyuo vya elimu ya juu vinawajibu mkubwa wa kuhakikisha wanatoa elimu kuhsu kupambana na vitendo vya kikatili kwa wanafunzi