Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:30 am

NEWS: RPC MAMBOSASA AWAFUNDA WAANDISHI

Dodoma: KAMANDA wa jeshi la polisi mkoa wa Dodoma SACP Lazaro Mambosasa amesema hisia za wanahabari na vyombo vya habari kujihisi kuwa ni kioo cha jamii ndio sababu kubwa ya kuingia kwenye uhasama na jeshi hilo.

Akiwahutubia wanahabari mkoani hapa katika maazimisho ya siku ya uhuru wa habari,Kamanda mambo sasa amesema hisia za wanahabari kujiona wanajukumu la kuonyesha vitendo vyote vya vilivyo kinyume na maadili upelekea wengine kuvuka mipaka.

“Hisia hizo za kubebe jukumu la msingi wengine wanalitumia vibaya kuandika na kutangaza habari za uchochezi ambazo uhatarisha amani utulivu na usalama,”alifafanua.

Kamanda Mambosasa amesema jeshi la polisi linawajibu kikatiba kulinda ulinzi na usalama wa nchi hivyo linapoingia kutimiza wajibu wake ndipo linapokutana na waandishi.

“Hapo ndio tunapokutana na waandishi nao uhisi kama tunawaonea hali inayopelekea kuharibu mahusiano yetu”.