- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RPC ILALA AKANUSHA KUMKAMATA MWANDISHI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala Zuberi Chembela, amekanusha taarifa za kukamatwa kwa mwandishi wa habari za kichunguzi Bollen Ngetti, anayedaiwa kukamatwa jana Agosti 8 na kupelekwa kituo cha polisi cha Stakishari.
Kamanda Chembela akiongea na mwandishi wetu amesema, hana taarifa za kukamatwa kwa mwandishi yoyote yule wa habari katika kituo hicho cha Stakishari na kwamba amekuwa akipigiwa simu zinazohoji kukamatwa kwa mwandishi huyo mara kadhaa kitu ambacho si cha kweli.
''Hakuna taarifa za kukamatwa kwake, afu wiki mbili tatu zilizopita nilipigiwa tena simu kuulizwa juu ya huyo huyo mwandishi Bollen Ngetti kama sisi tunamshikilia, niliwauliza hizo taarifa mmezitoa wapi, niliambiwa eti kwenye mitandao ya kijamii, mimi sina taarifa hizo ila wacha nifuatilie ili nijue kama Bollen Ngetti ni kweli yupo Stakishari'' amesema kamanda Chembela.
Taarifa za kukamatwa kwa mwandishi huyo zilianza kusambaa siku ya Agosti 8, kwa madai ya kwamba amekamatwa na askari watatu, na kupelekwa kituo cha polisi Stakishari.