- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RIZIKI LULIDA AITAKA SERIKALI KUITUMIA HIFADHI YA SELOUS KWA KUITANGAZA
DODOMA: MWENYEKITI wa kusimamaia Mzingira,Urithi wa Dunia na Wanyamapori ndani ya Bunge Riziki Lulida ameitaka Serikali kuitumia Hifadhi ya Selous ambayo inaonekana haijatumika katika kipindi cha zaidi ya miaka 50 .
Hifadhi hiyo ya Selous kwa sehemu kubwa ipo katika mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii,Lulida alisema,kutumika kwa hifadhi hiyo kutaiongezea Serikali mapato lakini pia kutawanufaisha kiuchumi wananchi wa mikoa inayoizunguka Hifadhi hiyo.
Alisema,Selous ni mbuga ya kwanza kwa ukubwa Duniani ambayo ina mapitio ( korido ) ya tembo kutoka Mozambiq kwenda Tanzania na kurudi kila mwaka .
Lulida ambayeni Mbunge wa Viti Maalum (CUF) kutoka mkoa wa Lindi alisema,Hifadhi ya Selous ukubwa wake ni mara kumi zaidi ya Hifadhi ya Serengeti ambayo ina ukubwa wa skwea mita za mraba 12 ,500 ,lakini kordo ya Selous Niassa ina ukubwa skwea mita za mraba 154,000 .
"Ujiulize kwanini miaka 50 mbuga hii haijatumika ,eneo hili linaonekana ni shamba la Bibi ,misitu inakatwa ,madini yanachimbwa ,korido inakuwa hautimiki, matokeo wanyama wakiwemo tembo wanauawa ,
"Leo unakwenda Selous hakuna wanyama,tumepiga kelele kwa muda mrefu jibu hakuna,tunajiuliza kulikoni,Kusini inaachwa ikiwa na urithi mkubwa wa Dunia ." alisema Lulida
Alisema,kitendo cha kuiacha Selous ni kuacha kitu ambacho kingeweza kufanya uchumi wa nchi uwe mkubwa lakini pia wananchi wake kunufaika na miradi ya ujirani mwema kutika kwa wawekezaji.
"Tunepiga kelele kwenye madini mpaka Serikali imefunguka,sasa tunataka kupiga kelele kwenye maliasili hasa Selous , pato litakalopatikana katika Hifadhi hii litafaidisha Nchi lakini pia na mikoa ya Kusini iliyozunguka mbuga hiyo
Alisema,iwapo Setikali itasimamia Hifadhi hiyo kikamilifu,pato lake litakuwa kubwa kuliko linalopatikana katika Hifadhi ya Serengeti kwa kuwa watalii watakuwa wanakwenda kule .
"Lakini leo hii mtalii anapewa ' package' kwenda Ngorongoro,Serengeti na Zanzibar,kwa nini asiende Kilwa na Lindi na sisi tukaambulia mapato ya kiuchumi?" alihoji Mbunge huyo