- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RIPOTI ZA HAKI ZA BINAADAMU DUNIANI ZAIKOSOA VIKALI TANZANIA
NAIROBI: Mashirika ya haki za binadamu Duniani ya Amnesty International na Human Rights Watch yametoa ripoti yao leo Octoba 28, 2019 mjini Nairobi nchini Kenya zikitoa shutuma kali kwa Tanzania juu ya ukandamizwaji wa waandishi wa habari, haki za binaadamu, watetezi wa haki za binadamu pamoja na vyama vya upinzani, wakidai ukandamizaji huo umeongezeka tangu 2015. (Anaandika Merry M. Mgawe kutoka Nairobi @MuakilishiPublisher).
Ripoti hizo mbili tofauti kwapamoja zimebainisha kuwa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli imebariki na kutekeleza sheria za ukandamizaji ambazo zinabana uandishi huru wa habari na kuweka sheria kuzuwia shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali na wanasiasa wa upinzani.
"Huku Rais Magufuli akitarajiwa kutimiza mwaka wanne mamlakani mwezi ujao, hatunabudi kuwa makini kutathmini rekodi ya serikali yake ya unyanyasanyasaji usiojali mfumo wa haki za binadamu ," amessma Roland Ebole, mtafiti wa Amnesty International nchini Tanzania. "Serikali yake inapaswa kuondoa sheria za ukandamizaji zinazotumiwa kuwakamata wapinzani, na kumaliza haraka ukiukaji wa hakiza binadamu na dhuluma ."amesema.
Hali ya waandishi wa habari nchini Tanzania?
Hii ni pamoja na kesi ya mwandishi wa habari maarufu wa habari za uchunguzi Eric Kabendera. Kabendera ambaye amekuwa akiandika taarifa kwa ajili ya vyombo mbali mbali vya habari yakiwemo magazeti ya Times and the Guardian nchini Uingereza mnamo mwezi Julai alikamatwa na kushtakiwa kwa makosa mkiwemo kujihusisha na genge la uhalifu na uhujumu wa uchumi nchini, kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya milioni mia moja za kitanzania, ambayo mawakili wake wameyakana wakidai yamechochewa kisiasa . Tangu wakati huo amekuwa gerezani.
Kesi kama vile ile inayomkabili Eric zimesababisha hofu miongoni mwa waandishi wa habari.Wengi miongoni mwa waandishi wa habari waliiambia BBC kuwa wanahofia kufuatilia taarifa zozote zenye utata kwa kuhofia upipizaji kisasi.
Ann Pinoni, mke wa mwandishi wa habari wa Tanzania Azory Gwanda ambaye alitoweka November 2017. Kabla ya kutoweka kwake Azory alikuwa akichunguza msururu wa matukio ya kutoweka kwa kwa watu katika eneo hilo .
Mke wake alimuona kwa mara ya mwisho akiwa nyuma ya gari jeupe, akiwa na watu wanne. Vyanzo ambavyo havikutaka kutaja majina yao vililiambia Shirika la kulinda waandishi wa habari CPJ kuwa wanaume waliokuwa na Azory walikuwa ni maafisa usalama.
Licha ya shinikizo za makundi ya haki za binadamu kuwataka polisi kuanza uchunguzi rasmi juu ya kutoweka kwa Azory, Mke wa Azory -Pinoni anasema familia bado inahangaika kuelewa ni nini kinachoendelea katika mchakato huo .
" Ninajaribu kuongea lakini sijui hata niongee nini. Sijui la kusema kwasababu wajibu nilionao kwa sasa ni mzito sana kiasi kwamba huwa kila mara nafikiria mume wangu na msaada ambao angekuwa ananipa . Lakini ninaendelea kuhangaika na maisha kwani sina chaguo . Mmoja wa watoto wangu yuko katika chuo cha sheria kwa sasa na ndiye aliyeathiriwa zaidi. Kila wakati Eanapowaona watu wengi wakinitembelea, anafikiri kuwa ninaficha ukweli kwamba baba yake amekufa. Ninajaribu kumliwaza lakini inaniumiza sana."
Mapema mwaka huu, Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania aliiambia BBC kuwa Azory alikuwa ni miongoni watu ambao walitoweka na kufa. Hata hivyo baadae alisema katika kauli yake kwamba kauli zake zilieleweka vibaya na kwamba hajui kama Azory alifariki: Palamagamba: 'Azory Gwanda alitoweka na kufariki'
Wakati Magufuli alipoingia madarakani , aliapa kukabiliana ufisadi. Mtindo wake wa uongozi ulimfanya alitwe Tingatinga au Bulldozer. Lakini wakati wa utawala wake, Tanzania imeshuka katika kipimo cha Uhuru wa vyombo vya habari kwa sasa ikiwa nafasi ya 118 kati ya nchi 180.
Waziri wa Habari Harrison Mwakyembe alipuuzilia mbali shutuma za kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari akisisistiza kuwa sheria mpya za vyombo vya habari zilizopitishwa hivi karibuni zinalenga tu kukabiliana na taarifa gushi.
" Ngoja niwakumbushe kuwa kuna sheria mpya hususan kwa mabloga wa mtandao na wale wanaosambaza taarifa gushi, msianze kulalamika kwamba serikali inanyamazisha vyombo vya habari. Kama ukisoma vipengele katika sheria utaona kuwa ni wazi vinazuwia uchapishwaji wa taarifa gushi. Lazima mfuate sheria kwasababu tumekuwa wavumilivu sana kwa muda mrefu . Sasa ninawaonya, Tunaanza kuchukua hatua ."
Lakini afisa wa CPJ Muthoki Mumo anaamini kuwa maagizo haya yenye onyo yanatoka kwa maafisa wa serikali yanaenda kinyume na agenda za Magufuli za awali.
''Ni nani atawawajibisha maafisa ambao hawafanyi kazi yao ipasavyo? ama atakayewajibisha wale wanaokula rushwa ? Ni nani atakayefichua uozo ambao Magufuli anasema anajaribu kukabiliana nao? Unahitaji kuwa na vyombo huru vya habari iki kufikia malengo ambayo serikali imejiwekea yenyewe. Kwa hiyo ni kama serikali inatuma ujumbe tofauti na unaokinzana. Kwa upande mmoja hakuna nafasi ya vyombo huru vya habari na kwa upande mwingine tunataka kuwa serikali ambayo inakabiliana na ufisadi ambayo inafikia mambo haraka na hauwezi kutuma ujumbe wa aina mbili kwa wakati mmoja, kwasababu mambo haya utendaji bora katika serikali, vita dhidi ya rushwa nsa vyombo huru vya havbari ni mambo yanayokwenda pamoja . "