Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 1:46 pm

NEWS: RIPOTI YAZIDI KUWAUMBUA VIGOGO WA CCM

DODOMA: KAMATI teule za bunge za kuchunguza madini ya Almasi na Tanzanati zimewasilisha ripoti hiyo kwa Spika wa Bunge Job Ndugai huku baadhi ya vigogo wakiwa wamekalia kuti bovu.

Ripoti hizo mbili zilizowasilishwa leo bungeni ziliwataja vigogo wakiwemo,Mawaziri kwa sasa ,waliokuwa mawaziri pamoja na aliyekuwa mwanasheria wa serikali.

Wenyekiti wa kamati hizo amewataja, baadhi ya vigogo akiwemo aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, aliyekuwa mwanasheria wa serikali Fredrick Werema, Waziri wa Tamisem,George Simbachawene,Prof.Sosper Mhongo,Edwin Ngonyani pamoja na watendaji mbalimbali wa serikali.


Kamati hizo za uchunguzi wa madini ya almasi na Tanzanite zimekuwa mwiba mkali kwa baadhi ya vigogo wa serikali pamoja na baadhi ya viongozi wakubwa ambao ni wastaafu.

Katika kamati ya Almasi iliyowasilishwa na Mussa Azzani Zungu hivyo taarifa ya Almasi, imesikitishwa na kampuni ya uchimbaji wa almasi kumzawadia kiongozi mkubwa ambaye alikuwa serikalini almasi yenye thamani ya dola milioni 20.

Mwenyekiti wa kamati ya ufuatiliaji katika ufuatiliaji masuala ya Almasi,Azan Zungu kuwa kamati imebaini kuwepo kwa madudu mengi katika uchimbwaji wa madini wa almasi.

Amesema kuwa licha ya kuwa kuna madudu mengi lakini bado maeneo mengi ya uchimbwaji wa madini ya Almasi hayajafanyiwa utafiti wowote.

Amesema taratibu ya uchimbaji wa almasi unafanywa kiholela huku Zungu amesema kuwa bado kampuni nyingi zimekuwa vinara wa kukwepa kulipa kodi au kubadilishana majina ya makapuni kwa madai ya kusingizia kupata hasara.

Akizungumzia kampuni ya uchimbaji wa madini ya Williamson, tangu mwaka 2007 hadi 17 haijawai kulipa mapato kwa kulipa kodi.

Amesema kuwa kuwa kampuni hiyo haikuweza kulipa kodi na Mrabaha kwa kisingizio kuwa kampuni inapata hasara,huku akihoji kuwa kama kweli kampuni inapata hasara kwanini isifunge virago.

Hata hivyo kamati imebaini kuwepo kwa taarifa tofauti kuwa na taasisi za serikali ambazo zinahusika katika sekta ya madini.

Pia kamati imesema kuwa madini mengi ya almasi yamekuwa yakiuzwa bila kulipia kodi huku nchi ikiwa imetumia pesa nyingi ambazo zingeingizwa katika maendeleo ya nchi.

Bilioni saba na milioni miasaba hazikuweza kuingia serikalini badala yake zimeweza kuingia katika mifuko ya wajanja.

Alisema licha ya kuwa almasi ya Tanzania kuwa bora kuliko sehemu nyingine lakini bado serikali imekuwa hainufaiki na jambo lolote kutokana na madini ya almasi.

Kamati ya Zungu imempata Prof.Mruma na hatia ya kuruhusu madini ya Almasi yapotee kizembe wakati akiwa Mwenyekiti wa bodi ya uwakala wa ukaguzi wa madini Tanzania (TMAA).

Zungu alisema Profesa Mruma alipohojiwa aliiambia kamati kwamba alisaini bila kusoma documents. Alipoulizwa kwanini alisaini bila kusoma, alisema alikuwa 'busy' sana na hivyo hakupata muda wa kusoma documents na hivyo aliamua kusaini kwa kuwa aliwaamini watendaji wa wizara.

Kamati zote mbili zimempata Simbachawene na hatia ya kusaini Mikataba yenye madudu mengi yaliyoingiza nchi kwenye hasara kubwa. Simbachawene ni moja wa watu ambao walisha wahi kufanya STAMICO.

Aidha Zungu amesema kuwa Waziri Muhongo alisaini mkataba wa Tanzanite na kampuni ya TML licha ya kushauriwa na mwanasheria mkuu na mwanasheria wa wizara asisaini.

Amesema kuwa Muhongo aliapishwa Uwaziri tarehe 24,na tarehe .29 akaenda ofisini kwa mara ya kwanza.

Halafu tarehe 31 akasaini Mauzo ya hisa kwa kampuni ya TML huku kukiwa na hati chafu za kiuhasibu. Yani kazi ya kwanza aliyofanya Muhongo baada ya kuapishwa ni kusaini mkataba ulioliingizia taifa hasara. Jiulize nini kilimkimbiza kusaini?.

“Makampuni mengi ya kigeni yanayochimba madini ya tanzanite na almasi hayajasajiliwa nchini. Yamesajiliwa katika nchi yanakotoka, lakini hapa nchini hayajasajiliwa BRELA. Hayatambuliki. Lakini yana operate. Can u imagine” alisema

KAMATI imebaini kuwa kwenye vyumba ambavyo almasi uwa inaifadhiwa kuna milango ya dharura ambayo utumiwa vibaya.

Serikali inapata hasara kubwa kutokana na usafirishaji wa almasi nje ya nchi ambao udaiwa kuwa inapungua thamani.

Kamati imeona kuwa kuna haja usafirishaji wa mwisho wa madini ya almasi ufanyike hapa nchini kwani haitaji uwekezaji mkubwa.

Kutokana na kukosa mapato stahiki kuna haja ya serikali kupitia misamaha yote ya kodi ya madini ya almasi hapa nchini.

Thamani ya madini ya almasi yanayouzwa nje ya nchi ni kubwa zaidi ukilinganisha na kodi inayolipa hapa nchini.

Viongozi wa serikali wailiopendekeza mgodi usinunuliwe ndio waliopendekezwa kuwa wajumbe wa bodi.