- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RIPOTI YA LHRC "UKATILI WA KINGONO NA UBAKAJI WAONGEZEKA NCHINI"
Dar es Salaam. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC) imetoa Ripoti ambayo inaonesha haki za binadamu kuanzia Januari hadi Juni 2019 ubakaji na ukatili wa kimwili kwa watoto na watuwazima kuzidi kushika kasi nchini Tanzania.
Ripoti hiyo iliyotolewa leo Jumanne Agosti 20, 2019 na Kituo hicho cha sheria inaonyesha Tanzania Bara asilimia 66 ya matukio ya ukatili dhidi ya watoto ni ubakaji wakati ukatili wa kimwili ukiwa asilimia 34.
Akisoma ripoti hiyo mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga amesema wafanyaji wakuu wa ukatili huo ni watu wa karibu wakiwemo wazazi, ndugu, jamaa, majirani na walimu.
Amesema asilimia 38 ya matukio ya ukatili kwa watoto yameripotiwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa huku Kanda ya Nyanda za Juu Kusini hasa Mbeya, Njombe na Iringa ikiwa ni asilimia 32.
"Upande wa Mwanza ulawiti wa watoto unaofanywa na watoto wenzao umeonekana kuwa changamoto katika kata 17 ikiwemo Igofo, Igoma na Nyegezi," amesema Henga.
Mtafiti wa LHRC, Fundikira Wazambi amesema suluhisho la ukatili huo ni kwa jamii kuongeza ulinzi kwa watoto bila kumwamini yeyote.
"Usiseme muda mwingi unatafuta fedha wakati mtoto wako wanaangamia, kama baba anaweza kumbaka mwanae vipi kuhusu jirani? juhudi za kulinda watoto ziongezeke," amesema.