- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RIPOTI YA CAG YABAINI UPIGAJI WA BILIONI 2.5
Dar es Salaam. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini Tanzania (CAG) ya mwaka unaoishia June 30, 2019 imebaini matumizi ya Sh2.58 bilioni yaliyofanywa kinyuma na sheria na Wizara ya Maliasili na Utalii nje ya bajeti na kabla ya kupitishwa na Bunge pia.
CAG amesema kuwa Fedha hizo zimetumika kwenye kampeni ya Urithi Festival Celebration na Channel maalum ya kutangaza vivutio vya utalii ya TBC Safari kinyume na utaratibu.
“Nilipitia matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii na kubaini kiasi cha Sh2.58 bilioni kimetumika kuanzisha chaneli ya Televisioni “Urithi Festival” ili kutangaza vivutio vya utalii,” imeeleza ripoti hiyo.
Imeeleza kuwa katika kutambua chanzo ya kugharamia matumizi hayo, hayakuwa na kifungu cha bajeti kama ilivyopitishwa na Bunge.
Imeeleza kuwa fedha hizo zilitolewa katika vifungu vingine vya matumizi ya wizara na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo ambazo ni Tanapa, NCAA, Tawa na TFSA.
“Nilijulishwa kuwa bajeti ya Urithi Festival ilipitishwa na menejimenti ya Wizara katika vikao mbalimbali vilivyofanyika,” inaeleza taarifa hiyo.