- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: RC MWANRI AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA IGUNGA
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amemsimamisha kazi Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wa wilayani Igunga John Mgeni kwa tuhuma za kudai rushwa ya Sh. milioni 2 kutoka kwa mfanyabiashara mmoja wa Mkoa huo.
RC Mwanri alifikia uamuzi wa kumsimamisha kazi Mgeni jana juni 24, 2019 baada ya mfanyabiashara mmoja kulalamikia alikutwa na kosa la kutotoa stakabadhi ya mauzo ya Sh10,000 na kutakiwa kulipa faini ya Sh4.5 milioni au kupelekwa mahakamani. Ilidaiwa meneja huyo alimwambia mfanyabiashara huyo anaweza kumpa Sh2 milioni ili asipelekwe mahakamani wala asilipe adhabu inayohitajika Kisheria.
Mwanri alitoa amri ya kusimamishwa wakati wa semina ya uelimishaji wa wafanyabiashara kuhusu ulipaji wa kodi, iliyofanyika wilayani humo.
Kutokana na tuhuma hizo, Mwanri aliiagiza Taasisi za Kuzuia na Kudhibiti Rushwa (Takukuru) kufanya uchunguzi na kumtaka meneja huyo kutoingia ofisini mpaka utakapokamilika. Kwa upande Meneja wa TRA Mkoa wa Tabora, Thomas Masese aliwataka wafanyabiashara kuwa huru kufichua watendaji wa mamlaka hiyo wanaofanya kazi kinyume cha sheria.